Ni siku chache tuu mara baada ya serikali Mkoani Mwanza kufanya Oparesheni maalum ya kuwaondoa wafanyabiashara wadogo katikati ya Jiji kumekuwepo na taarifa za baadhi ya wafanyabiashara kutishia kuchoma moto maduka ya wafanyabiashara ambapo serikali imetoa onyo kali kwa watu watakao husika huku ikidaiwa baadhi ya askari mgambo wa Halmashauri ya Jiji walioshiriki katika oparesheni ya kuwaondoa kupokea kipigo kutoka kwa wafanyabiashara hao.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Mary Tesha, amesema Serikali haitakuwa tayari kuvumilia vitendo hivyo, vinavyoendelea kutekelezwa na baadhi ya wafanyabiashara, kama njia ya kulipiza kisasi cha kuhamishwa katikati ya Jiji.
Mary Tesha ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana na hapa katika video hii anasikika BOFYA PLAY.
Ni siku ya tatu sasa tokea kufanyika kwa operesheni hiyo maalum ya kuwaondoa wafanyabiashara wadogo katika maneo ya katikati ya mji na kupelekwa maeneo rasmi ambayo ni kiloleli, Buzuruga, Nyegezi pamoja na eneo la Temeke kata ya Nyakato.
NA. Zephania Mandia wa gsengoblog
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.