Mshambuliaji wa timu ya vijana ya Mbao Fc U-20 Ismail Mrisho Khalfan anayevalia jezi nambari 4 amefariki Dunia jioni hii baada ya kuanguka Uwanjani Kaitaba wakati wa Mtanange wao dhidi ya timu ya vijana wa Mwadui ikiwa ni mechi ya mwisho ya kumaliza duru la kwanza la ligi ya Vijana.
Ismail Mrisho Khalfan amefariki akiwa na miaka 19.
Mshambuliaji wa timu ya vijana ya Mbao Fc U20 Ismail Mrisho Khalfan anayevalia jezi nambari 4 amefariki Dunia jioni hii baada ya kuanguka Uwanjani Kaitaba wakati wa Mtanange wao dhidi ya timu ya vijana wa Mwadui ikiwa ni mechi ya mwisho ya kumaliza duru la kwanza la ligi ya Vijana.
Ismail Khalfan amefariki akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mjini Bukoba.
Mrisho Halfan ndie aliyeifungia bao la kwanza na bao la pili lilifungwa kwa mkwaju wa Penati hivyo mtanange kumalizika kwa 2-0.
Ismail Khalfan kabla ya kufikiwa na umauti aliweza kuifungia timu yake bao la kwanza na bao la pili lilifungwa kwa mkwaju wa Penati hivyo mtanange kumalizika kwa 2-0.
Kabla ya kuanguka Ismail aligongana na beki wa Mwadui Fc na baadae akiwa peke yake alianguka chini lakini akainuka halafu akaanguka tena na kutokana na ukosefu wa huduma ya kwanza na gari la wagonjwa Katika Uwanja wa Kaitaba kulipelekea marehemu kupandishwa kwenye gari la zima moto na kupelekwa hospital ambapo mauti yalimkuta.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.
Hivi ndivyo mtanange ulivyokuwa Uwanjani Kaitaba jioni hii.
Ismail Mrisho Khalfan ndiye aliyeifungia bao la kwanza Mbao FC. Na hapa akishangilia bao lake la kwanza kwa aina yake kwa Timu ya Mbao Fc.
Ismail Mrisho Khalfan(kulia)
Vijana wa Mbao Fc walianza kipindi cha kwanza wakiwa kwenye hali ya kutaka kuibuka na ushindi
Ismail Mrisho Khalfan(kulia) akimkacha mchezaji wa Mwadui fc
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.