Meneja wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti akiwaonesha wanahabari (hawapo pichani) Dar es Salaam leo, moja ya picha ya ndege 22 za zamani zitakazotua nchini Novemba 28, mwaka huu, kwa mashindano ya 'Vintage Air Rally' yenye lengo la kutangaza utalii. Ndege hizo zilitengenezwa kati ya mwaka 1920 na 1930.Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Mafuta ya Ndege wa kampuni hiyo, Raymond Tungaraza. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Meneja wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti akiwaonesha wanahabari (hawapo pichani) Dar es Salaam leo, Nchi za Afrika ikiwemo Tanzania ambamo Mashindano ya Ndege 22 za zamani 'Vintage Air Rally' zilizotengezwa kati ya mwaka 1920 na 1930 zitatua na kutangaza utalii pamoja na kukusanya fedha za misaada kwa jamii. Kulia ni Meneja Rasirimali Watu wa kampuni hiyo, Loveness Hoyange.
Meneja wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti (katikati) akizungumza katika mkutano na wanahabari (hawapo pichani) Dar es Salaam leo, kuhusu maandalizi wa mashindano ya Ndege 22 za zamani 'Vintage Air Rally' zilizotengezwa kati ya mwaka 1920 na 1930 zitakazotua nchini Novemba 28 na kutangaza utalii pamoja na kukusanya fedha za misaada kwa jamii. Kulia ni Meneja Rasirimali Watu wa kampuni hiyo, Loveness Hoyange na Mkuu wa Idara ya Mafuta ya Ndege wa kampuni hiyo, Raymond Tungaraza.
Mkuu wa Idara ya Mafuta ya Ndege wa kampuni hiyo, Raymond Tungaraza.akijibu maswali ya wanahabari
Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Mafuta ya Ndege ya kampuni hiyo, Andrew Lauwo (kulia) akifafanua jambo katika mkutano huo
Mkutano ulivyokuwa
Puma Energy
Tanzania Ltd
Kampuni
ya puma kuwa mwenyeji wa mashindano ya ndege za zamani
23rd November 2016
Taarifa Kwa
umma
Kampuni ya Puma Energy
Tanzania ambayo ni sehemu ya Puma Group, Kampuni ya kimataifa
inayojishughulisha usafishaji mafuta ghafi, kutunza na kusambaza mafuta
yaliyosafishwa tayari kwa matumizi, inayofuraha kujulisha umma kuwa itakua
mfadhili mahsusi katika mashindano ya anga yanayohusisha ndege za
zamani kwa mwaka 2016.
Vintage Air Rally inahusiaha
ndege za zamani za miaka ya 1920 na 1930 ambazo zinarushwa na marubani wenye
uzoefu mkubwa kutoka sehemu mbalimbali duniani, wakiruka kukatisha Afrika
kuanzia kisiwa cha Crete Ugiriki hadi Cape town Afrika ya kusini.
Shindano hili lilianza tarehe
12/11/2016 kule Crete, Ugiriki na safari yote itachukua siku 35 katika jumla ya nchi 10 ambazo ni Ugiriki,
Misri, Sudan, Ethiopia, Kenya, Tanzania, Zambia, Zimbabwe, Botswana na Afrika
ya Kusini.
Shindano hili linalengo la
kutahini ujuzi wa marubani husika, na
wakati huohuo kuchangisha fedha kwa ajili ya mashirika ya Kimataifa ya hiari
UNICEF, Bird life International and Seed Bombing. Sisi kama Puma tunasikia
fahari sana kuwa sehemu ya uvumbuzi huu wa ajabu.
“Kampuni ya Puma
Energy inayofuraha kuwa mwenyeji wa mashindano haya. Ndege zinazotumika katika aina hii ya
mashindano huwa zinahitaji aina maalumu ya matengenezo kwa kuzingatia umri wake
pamoja na teknolojia iliyotumika. Tumejikita katika kuendela kufanya vyema na
pia kuwa na uhakika wa uapatikanaji wa bidhaa ya mafuta na tunafuraha kutoa
mchango wetu katika kuhakikisha kwamba mashindano yanayafanyika vyema. Jukumu
letu katika kusaidia
kuendeleza utalii ndani ya
nchi yetu linabaki kuwa sehemu muhimu sana katika masula yetu ya kijamii kama
kampuni katika kutimiza majukumu yetu ya kila siku”, Alisema Philippe Corsaletti,
Meneja Mkuu wa Puma Enery Tanzania.
Vintage Air Rally watatua Tanzania (KIA) tarehe
28/11/2016 wakitokea uwanja wa ndege wa Wilson Nairobi. Marubani watakua na
muda mzuri wa kutembelea mbuga zetu za wanyama kama sehemu ya safari yao. Hili
pekee pia litasaidia katika kuweka utalii wa nchi yetu katika mtizamo wa
kimataifa Zaidi kwani shindano hili linafuatiliwa na maelfu ya watu katika
maeneo mbalimbali duniani.
Kampuni ya Puma Energy Tanzania imejiandaa kabisa
kupokea ugeni huu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha huduma zote za kujaza mafuta
ili kuhakikisha urukaji ulio salama. Ndege hizi zinatumia mafuta aina ya Avgas
ambayo kwa sasa ni kampuni ya Puma pekee inayotunza hapa nchini. Timu ya watu
wetu imejiandaa kupokea na kuhudumia msafara mzima katika kiwanga cha juu cha
ubora na ufanisi. Uwepo wa bohari zetu za mafuta ya ndege katika maeneo
mbalimbali nchini unafanya iwe rahisi kuhudumia ndege hizo ambao msafara huu
utapita.
Kwa hapa Tanzania, Vintage Air Rally Aircrafts zitajaza
mafuta Kilimanjaro, Arusha, Dar es salaam, Zanzibar, Dodoma, and Songwe kabla
ya kuelekea Zambia ambapo watapokelewa na kuhudumiwa na wenzetu wa Puma Zambia.
Tanzania
itaweka historia kwa kuwa moja ya nchi chache duniani ambapo mashindano haya yatapita.
“Tunawakaribisha wananchi wote katika tukio hili la kihistoria wakati ndege za
Vintage zitakapokua zikipita maeneo yenu na kutumia fursa hii kuendeleza utalii”,
Alisema Ndugu Philippe.
Kuhusu njia itakayotumika:
Njia
inayotumika ni sawa kabisa na ufuatishaji wa safari ya shirika la ndge la
Imperial ya mwaka 1931 “safari ya Afrika” ambapo ndege itakua ikiruka chini
kupitia Nile kutokea kongo hadi Khartoum, kupitia nyanda za juu za Ethiopia,
uwanda wa chini wa Kenya, na hatimaye
sehemu yenye changamko sana ya Afrika Mashariki. Baada ya hapo itaondoka tena kupitia
Kilimanjaro hadi Serengeti, na hatimaye hadi kwenye visiwa vya marashi ya
Zanzibar na hadi chini Zaidi, kupitia Zambia, juu ya maporomoko ya Victoria,
hadi Bulawayo Zimbabwe. Siku za mwisho za safari hii ndefu inayohitaji pumzi
nyingi itawafikisha Botswana na Afrika ya Kusini - Capetown ambapo utakua
mwisho wa safari
Kampuni ya Puma Energy ni
kampuni ya kimataifa ya viwango vya kati ambayo imejikita katika kusafisha
mafuta ghafi, kutunza na kusambaza mafuta masafi kwa watumiaji katika zaidi ya
nchi 45 duniani. Puma Energy iliingia Tanzania mwaka 2012 na hadi sasa
inaongoza katika soko na pia kampuni
pekee yenye uwepo katika viwanja vinane hapa Tanzania ambavyo ni Kilimanjaro, Zanzibar, Songwe,
Mwanza, Tabora, Dodoma, Arusha, na Julius Nyerere.
Philippe Corsaletti
Meneja Mkuu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.