Thursday, November 24, 2016
|
Ndani ya studio za Jembe Fm waratibu kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza walipo fanya mahojiano na kipindi cha Drive Mixx chini ya watangazaji Harith Jaha (kulia) Joyce Ngerangera (mbele) na Chriss The Dj mtamboni. |
Tangu jana hata leo Jiji la Mwanza limepokea zaidi ya wadau 500 kutoka miji ya ukanda wa Ziwa Victoria, wakitoka katika Halmashauri zipatazo 130 kwa madhumuni ya kuziainisha fursa na rasilimali zilizopo Kanda ya Ziwa, jinsi ya kukabiliana na changamoto zilizopo na hata za baadae, pamoja na kushughulika katika huduma za usafi, kutoa misaada kwa hospitali na upandaji miti.
Baadae jioni wajumbe wataungana kwenye mkutano kisha chakula cha jioni. @jembefm ni moja kati ya wadhamini wa kusanyiko hili. CC:- #DriveMix #SEGA_LA_LEO @mustafakinkulah @johangasa4 #KAZINANGOMA @mansourjumanne @djscopion Yaani ndiyo kusema #VyumaVimekaza
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.