Wilaya za Ilemela na Nyamagana jijini Mwanza zimetoa muda wa siku saba kuanzia novemba 23 hadi disemba 3 kwa wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kwa jina la Machinga kuondoa biashara zao maeneo yasiyoruhusiwa katikati ya jiji hilo huku wafanyabiashara hao wakidai hawana taarifa za wao kutakiwa kuhama.
Wakizungumza na Gsengo Blog leo jijini Mwanza , wakuu wa wilaya hizo Mary Tesha na Dr. Leonard Masale, wamesema endapo wafanyabiashara hao watakaidi kuondoka katika muda uliopangwa wataondolewa kwa nguvu.
Machinga hao wamesema hawawezi kuhama kwakuwa maeneo waliyopangiwa siyo rafiki kwa biashara zao pia hakuna miundombinu hivyo wanaiomaba serikali kuwaacha waendele na biashara katika maeneo waliopo sasa.
(MSIKILIZE MMOJA KATI YA MACHINGA - REVOCATUS DAUDI)
Kwa upande wake m/kiti wa Shirikisho la umoja wa Machinga nchini(SHIUMA) Ernest Masanja amesema wamachinga wanaofanyabiashara zao katika eneo la Makoroboi wapo kisheria na kwamba hawana mpango wa kuhama.
Amri hiyo inayowataka wafanyabiashara hao kuhamia maeneo ya Nyegezi, Kiloleli na Buzuruga nje kidogo ya jiji la mwanza imetolewa ikiwa ni miezi mitatu tangu rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania John Magufuli aagize wafanyabiashara hao watengewe maeneo yaliyoko katikati ya jiji.
NA. ZEPHANIA MANDIA WA GSENGO BLOG.
ZAIDI: Sikiliza Kazi na Ngoma kesho Alhamisi ya tarehe 24Nov2016 saa 5 hadi saa 7 mchana, kupitia Radio Jembe Fm Mwanza.
NA. ZEPHANIA MANDIA WA GSENGO BLOG.
ZAIDI: Sikiliza Kazi na Ngoma kesho Alhamisi ya tarehe 24Nov2016 saa 5 hadi saa 7 mchana, kupitia Radio Jembe Fm Mwanza.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.