Akiwa jijini Mwanza leo mama samia atazindua kampeni ya kupambana na Saratani ya titi na mlango wa kizazi na kuzungumza na wakazi wa jiji la Mwanza katika viwanja vya Furahisha kabla ya kuelekea wilayani Sengerema.
Katika kile kinachoonekana ni kubana matumizi ya serikali ya awamu ya tano, makamu wa rais mama SAMIA SULUHU HASSAN ametumia ndege ya abiria kutoka DSM kwenda Mwaza kwa ziara ya kikazi.
Aidha Mama Samia akaeleza tajiriba yake ya kutumia ndege mpya za ATCL Bombardier DASH8-Q 400. BOFYA JIONEE KATIKA VIDEO.
Akiwa Mkoani Mwz Makamu wa rais mama samia anatarajiwa kuzungumza na wananchi katika viwanja vya Furahisha ambapo atazindua kampeni ya kupambana na saratani ya titi na shingo ya kizazi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.