Katibu tawala wa Wilaya ya Arusha Arusha David Mwakiposa akiwa anaongea na waendesha bodaboda wa wilaya ya Arusha
|
Na Woinde Shizza,Arusha
Baadhi ya Vijana wa
mkoa wa Arusha wanaofanya kazi ya
kuendesha bodaboda wamelalamikia kitendo
cha polisi wajulikanao kwa jina la Voda fasta kuwatoza rushwa kila kona pamoja na jiji kutowapa mikopo ya Vikundi
jambo ambalo wamedai linawanyima raha na uhuru wa kufanya kazi .
Hayo wamesema leo wakati mkutano baina yao na katibu tawala
wa Wilaya ya Arusha Arusha David Mwakiposa wakati alipokutana nao kusikiliza kero zao
zinazowakabili vijana hao ambao wanaendesha bodaboda
Mbali na kero hiyo pia wameilalamikia Halmashauri ya jiji la
Arusha kwa kushindwa kuwapa mikopo ambayo inaweza kuwasaidia kujiajiri wenyewe .
Mmoja wa vijana hao bodaboda ambae alijitambulisha kwa jina
la Daudi Molel alisema kuwa wamekuwa wakipata kero sana haswa kutoka kwa hawa
askari polisi wanaojulikana kwa jina la Vodafasta kwani wamekuwa wakiwakamata
hovyo na wamekuwa wakiwatafutia makosa mengi ili mradi tu wapewe rushwa.
“uanajua unakuta mimi nimeshusha abiria gafla wanakuja
anaanza kukutafutia makosa kibao ukikataa wanachomoa fungua wanaondoka nazokitu
ambacho sio kizuri kabisa na akirithishi kabisa ,mimi nimeajiriwa tajiri
amenituma fedha naitaji kupitia hiii hii bodaboda yangu nilishe familia
nivalishe sasa jamani wanavyotudai rushwa kila mahali wanapotukamata
wanatuhumiza sana tunaomba serikali itusaidie kwa hili “Alisema Asea Akyooo
Aidha aliongeza kuwa
kwa upande wa jiji wamekuwa wanatoa fedha za mikopo kwa kificho sana kwani wamekuwa wanatoa fedha hizo kwa
upandeleo na wanachagua vijana wa kuwapa na wao kama maderea bodaboda wamesahaulika
kabisa hivyo wanauomba uongozi usika wawafikirie na wao ili waweze kupata mikopo kwa ajili ya kujinunulia pikipiki zao binafsi
na waweze kujiajiri.
Akijibu hoja hizo katibu tawala wa wilaya ya Arusha David Makiposa aliwasihi
vijana hao kuunda vikindi na serikali ya wilaya ya Arusha ipo tayari
kuwasimamia kuhakikisha nao wananufaika
na pesa za mikopo ya jiji na serikali imeshatoa
maelekezo kwa uongozi wa jiji
kuhakikisha katika fedha watakazotoa kwa awamu hii wahakikishe kundi la boda
boda linapewa kipaumbele cha kipekee.
Alisema kuwa dhamira
ya dhati ya serikali ni kutatua kero za
wananchi kwa haraka iwezekanavyo ,hivyo azma ya serikali ya awamu ya tano ni kila kiongozi ama mtendaji anatatakiwa kutatua
kero zilizopo katika eneo lake ipasavyo ivyo hana sababu ya kukaa ofsisini wakati kuna maelfu
ya wananchi wanyonge wanateseka mtaani na wakiwa wanakabiliwa
na kero mbalimbalimbali.
Pia alitumia muda huo
kuwashukuru watendaji wa kata kwa
akuanza kutatua kero za wandesha bodaboda hao
na kuwaagiza wengine kwenda kuweka program maalumu za kukaa na bodaboda na kuwasaidia shida zao na aliaidi kuendelea kuwafatilia.
Aidha katika mambo
ambayo kikao hicho kiliazimia ni pamoja na kuundwa uongozi wa wilaya kila kata ,kanda ya wilaya ndani ya siku saba ili waendesha bodaboda
wapate chombo cha kuwasemea matatizo yao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.