ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, November 15, 2016

POLISI PWANI YANASA KILIMO CHA UMWAGILIAJI WA BANGI.

Pwani. 
Polisi mkoani Pwani imekamata viroba 251 vya bangi na vifaa vya kumwagilia mashamba ya zao hilo haramu.
Vifaa hivyo ni mashine sita za umwagiliaji na mipira yake zinazodaiwa zilikuwa zikitumika kwa kilimo cha zao hilo haramu. Idadi ya magunia yaliyokamatwa yakiwa na mbegu za bangi ni 32.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Boniveture Mushongi alisema katika msako walioufanya majira ya alfajiri ya saa 11:00 waliwakamata watu wawili, Msahiro Msahilo mkazi wa Usure na Hamisi Selemani anayeishi Gwata,  wakituhumiwa kumiliki bangi hiyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.