ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 26, 2016

HUAWEI, CLARA BOUTIQUE WAZINDUA DUKA KUBWA KANDA YA ZIWA.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Bruce Zhang (kulia) na Mkurugenzi wa Clara Huawei Smartphone Brand Shop, Clara Mwasa wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Duka hilo uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Bruce Zhang (kulia) na Mkurugenzi wa Clara Huawei Smartphone Brand Shop, Clara Mwasa wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Duka hilo uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Bruce Zhang (kulia) ikiwapungia mkono wageni waalikwa mara baada ya uzinduzi wa duka la Clara Huawei Smartphone Brand Shop lililoko jijini Mwanza. Kulia ni Mkurugenzi wa Duka hilo, ClaraMwasa.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Bruce Zhang (katikati) akiwaonyesha wateja walihudhuria uzinduzi wa Duka la Clara Huawei  Smartphone Brand Shop lililozinduliwa rasmi mwishoni mwa wiki jijini Mwanza. Kulia ni Mkurugenzi wa Duka hilo, Clara Mwasa.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 
Huawei, Clara Boutique  wazindua duka kubwa Kanda ya Ziwa  
Novemba 25, 2016:

Kampuni ya Teknolojia ya Mawasiliano ya Huawei Tanzania kwa kushirikiana na Mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza, Clara Salon & Boutique imefungua duka kubwa liitwalo “Clara Smartphone Shop” katika Jiji la Mwanza. Hatua hiyo ni mwendelezo wa Huawei katika kutekeleza moja ya mikakati yake ya kujitanua kibiashara nchini.

Huawei imeona kuwepo wa Duka hili kubwa la Clara, katika Jiji la Mwanza kunatokana na kukua mahitaji ya bidhaa za Huawei nchini na hivyo kutoa fursa ya watumiaji kupata huduma kwa karibu zaidi.

“Tunafahamu watanzania walio wengi wanachohitaji, ndiyo maana leo hii tuko Mwanza. Tunaamini kuwa hii ni fursa pekee kwa wakazi wa Mwanza na miji ya jirani kupata bidhaa zetu zenye ubora na viwango vya hali ya juu. Tunaamini kuwa Clara Salon & Boutique wana jina kubwa katika Jiji la Mwanza na hivyo itatusaidia sisi kutimiza lengo letu, anasema Mkurugenzi huyo.

Mwaka huu kampuni hii ya simu ilijipanga kusambaza huduma yao nchi nzima, sambamba na kufungua maduka kwaajili ya kusogeza huduma zetu kwa wateja. Hali hii imetuongezea wepesi wa utoaji wa huduma zao kwa kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kutambua mahitaji muhimu kwa wateja wetu.
  
Tanzania imefaidika na uhusiano mzuri uliopo kati yake na Huawei kwa kuwa na miradi mbalimbali yenye lengo la kuboresha teknolojia ya mawasiliano. Huawei inampango wa kukuza teknolojia ya mawasiliano nchini Tanzania na sasa imeanza kushirikiaba kwa karibu na wazawa kama Clara. Milango iko wazi kwa yeyote anayetaka kutuunga mkono kiabiashara.

Wakati Huawei inazindua duka hilo katika Ukanda wa Kanda ya Ziwa, Mkurugenzi huyo alitangaza uwepo wa simu mpya ya kisasa, Huawei Y3II na nyinginezo, katika soko la simu nchini.

Alisema kuwa simu hiyo ina ubora na kuwataka watanzania kutumia, akifafanua zaidi kuwa ni simu yenye ubora, lakini gharama yake sio kubwa, ikilinganishwa na simu za makampuni mengine.Pia bidhaa nyingine zitaambatana na simu hiyo kama matoleo mangine tofauti Huawei P9, Y3c, Y5II ,Y6II, Y3lite na nyingine nyingi.  

Hizi ndizo faida za kuwa na duka kubwa katika Jiji la Mwanza. Kuanzia sasa wanunuzi wa bidhaa zetu wana fursa ya kupata bidhaa zetu zote kwa wakati. Tunaanza na simu hii ya Huawei Y3II ambayo kwa hakika kila atakayeamua kuitumia ataipenda kwa ubora wake.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, Kampuni ya Huawei inaendelea na mchakato wake wa kusogeza huduma zake kwa wateja wake, kwa lengo la kutimiza malengo yake ili kupambana na soko la mawasiliano.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.