ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 26, 2016

HIZI HAPA SIMULIZI ZISIZO SAHAULIKA ZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO.


Kama umeikosa Stori ya #KAZINANGOMA kupitia JEMBE FM ukiwa na @mansourjumanne + @gsengo 👂Mama Anna amekuwa ndani ya Shirika la Kupambana na vitendo vya ukatili katika jamii toka kuanzishwa kwake mwaka 1999 akipitia matukio mengi aliyoyakabili na mengine kupambana nayo.

Hapa anatupa uzoefu wake wakulitumikia shirika hilo akisimulia mmoja ya matukio ambayo hato yasahau:- Mama aliyekatwa sikio na mumewe na kisha mumewe kuswekwa ndani na baada ya siku chache akafia mahabusu, ndugu wakacharuka na kumnyang'anya mali zote walizovuna na mumewe wakidai kuwa ndiye aliye muua. BOFYA PLAY KUSIKILIZA KISA MKASA.VIPI MIKASA YA UKATILI KWA WATOTO.... 

Mume alitelekeza familia yaani mke na watoto, baba akaenda mbali kuishi na kimada, sasa huyu mke aliyeachwa na watoto alikuwa anajiweza kwa biashara, hivyo maisha yakawa yanaendelea na kusonga kama kawaida huku watoto wakisoma kwa mwendo wa mafanikio.

Baba alivyoona hali hiyo ya viashiria vya mafanikio kwamba baadaye watoto wangepata elimu na kuja kumsaidia mama yao kiuchumi, alichokifanya ni kitendo cha ukatili usiovumilika ...baba akatuma ndugu zake wamvizie yule mtoto akiwa anatoka shule na kumlawiti ambapo walimuambukiza magonjwa ya zinaa. 

BOFYA PLAY KUSIKILIZA KISA KIZIMA.
aaa

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.