Msichana aliyezuiliwa kuingia darasani kutokana na kile kilichotajwa kuwa sketi fupi. |
Mwanafunzi mmoja nchini Uganda ,Joaninne Nanyange amechapisha ujumbe mrefu katika mtandao wake wa Facebook akilalamika vile alivyozuiwa kuingia katika mlango wa darasa lake la chuo kikuu siku ya Jumatano na wanawake wawili mmoja akiwa amevalia magwanda ya polisi.
Anasema askari huyo alimtaka kuvuta sketi yake chini hadi mwisho.
''Nilicheka kwa sababu ombi lake halikueleweka.Alisisitiza hivyobasi nikamwambia hapo ndipo mwisho na hakuna vile ningeweza kuivuta hadi chini''.
Ni hapo ndipo alipoelezewa kuwa sketi yake ni fupi na kwamba hangeweza kujiunga na wenzake katika darasa la kusomea uwakili.
Hatahivyo kitivo cha uwakili mjini Kampala kimesema kuwa hakijapokea malalamishi rasmi kuhusiana na tuki hilo.
Lakini msemaji wa kituo hicho amesema kuwa kuna maadili ya mavazi na kwamba wanawake wanafaa kuvaa sketi zinazofika magotini.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.