ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 26, 2016

BREAKING NEWS:- RAIS WA ZAMANI WA CUBA 'FIDEL CASTRO' AFARIKI DUNIA AKIWA NA UMRI WA MIAKA 90.

Aliyekuwa Rais wa zamani wa Cuba mwanamapinduzi wa Kikomunisti Fidel Castro, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90, hii ni kwa mujibu wa kaka yake.
"Kamanda huyo mwanamapinduzi wa taifa la Cuba alifariki mnamo majira ya saa 22:29 usiku wa tarehe 25 Novemba 2016 (03:29 GMT Saturday)," alisema Rais Raul Castro.
Fidel Castro amekuwa rais wa muda mrefu kuliko wote kwani ameiongoza nchi ya hiyo iliyokuwa ndani ya mfumo wa chama kimoja kwa takribani miaka 50 kabla ya rais wa sasa Bwana Raul ambaye ni kaka yake kuingia madarakani mnamo mwaka 2008. 
Wafuasi wake wamemtaja kuwa alikuwa mtu wa kuirejesha Cuba kwa wananchi yaani Serikali ilikuwa ni mtumishi wa wananchi. Lakini amekuwa akishutumiwa kuukandamiza upinzani. 
Fidel Castro, amekuwa mwanasiasa aliyeitawala Cuba kama Waziri mkuu tangu mwaka 1959 hadi 1976 na baada ya hapo akawa rais tangu mwaka 1976 hadi 2008 alipoachia madaraka baada ya afya yake kudhoofika.


Fidel Castro                                                                               Julius K. Nyerere
IMEANDALIWA NA GSENGO BLOG

Fidel Castro, ni mmoja ya wapigania uhuru na mwanamapinduzi duniani na kiongozi wa namna yake katika utawala, pia amekuwa kiongozi wa namna yake duniani aliye amini kuwekeza katika nguvu za kivita na afya nchini Cuba.

Alikuwa ni rafiki mkubwa wa Mwalimu J.K Nyerere enzi za utawala wake mnamo mwaka 1977, ambapo alikuja hapa nchini petu Tanzania kuonana na Mwalimu katika kuangaia namna ya kuendeleza suala la kilimo na tiba ambapo pia alitoa nafasi ya wataalamu wa Tanzania kupata mafunzo ya kilimo nchini Cuba.

Tangu mwaka 2006 alianzkupata maradhi na mwaka 2008 akang'atuka na kukabidhi madaraka kwa Raul Castro.

PUMZIKA KWA AMANI MPIGANAJI MWAMBA WA DUNIA FIDEL CASTRO.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.