Mkuu wa kitengo watu wenye tatizo la ugonjwa wa Usonji (National Association for People with Autism
–Head) Dkt Stella Rwezaula (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati
wa kuzindua warsha maalum kwaajili ya kuoa uelewa kwa watu mbalimbali kuhusu
tatizo la Usonji nchini, anaefuata ni Dialla Kassam ambaye ni kurugenzi wa
kituo cha Afya cha LOTUS ambao ndio wazamini wa warsha hiyo, akifuatiwa na
mtaalam wa mambo ya usonji dunia bw, Kevin Baskerville, kutoka Leicestershire,
UK, pamoja na Meneja wa kituo cha Lotus Bi Deepack Gorecha kushoto.
Wapili toka kushoto ni Mtaalam wa mambo ya
Usonji toka UK bw, Kevin Baskervile
akikabidhi mfumo maalum alioubuni kwaajili ya kusaidia kufundisha watoto wenye
usonji kwa dokta Stela Rwezaula toka muhimbili ili kusaidia kufundisha watoto
wanaopatwa na tatizo hilo kupata elimu kwa njia ya picha. katikati anaeshuhudia
ni mkurugenzi wa kituo cha afya kinachosaidia watoto wenye usonji Bi Dialla
Kassam na Deepak Gorecha (kushoto) wakishuhudia. Aliyesimama ni Mtaalam wa tatizo la Usonji toka UK bw Kevin Baskervile toka UK akitoa mada kwa wadau
mbalimbli wakati wa warsha maalum kwaajili ya kueneza uelewa kuhusiana na tatizo
la usonji nchini.
Wapili toka kulia ni mkuu wa kituo cha afya
kinachosaidia wagonjwa wa Usonji nchini Bi Dialla Kassam akiongea na waandishi
wa habari kuhusu udhamini wao wa warsha maalum ya kuongeza uelewa wa usonji kwa
wadau mbalimbali nchini wakiwemo wazazi, anaefuata ni mtaalam wa tatizo la
usonji toka UK bw, Kevin Baskerville, Meneja wa kituo cha afya cha LOTUS bi
Deepak Gorecha na Mkuu wa kitengo kinachoshughulikia watoto wenye usonji dkt
Stella Rwezaula.
- Usonji bado changamoto kubwa Tanzania
Tanzania bado inakabiliwa na
changamoto kubwa ya kukabiliana na ugonjwa wa usonji ambao wengi hawautibu
kutokana na kutoelewa dalili zake, imefahamika.
Hili lilielezwa na mkuu wa Chama
Cha watu wenye Usonji Kitaifa (NAPA-T) Dr Stella Rwezaula katika mkutanona
waandishi wa habari.
“Dalili za usonji bado
hazijafaamika vizuri kwa wazazi na walimu nchini hivi wanashindwa kuutibu
ugonjwa huu au kupata msaada wa kitaalamu kwani ni ugonjwa ambao una mambo
mengi yanayoathiri namana mtu anavyowasiliana na mara nyingi huwa na tabia ya
kufanya vitu kwa kurudia rudia bila kukusudia,” alisema.
Alisema kwa mwaka huu, kituo cha
Afya cha Lotus (LHC), ambacho sio cha serikali na kinafanya kazi za kusaidia
watoto wenye mahitaji maalumu, kimeifadhili NAPA-T kufanya warsha inayolenga
kutoa elimu kuhusu usonji na warsha hii itawaleta pamoja washiriki takriban 100
kutoka sekta binafsi na za kiserikali. “Hu ni moja wa mkakati wa LHC kutoa
elimu katika jamii na kuwaleta pamoja watoto na wazazi wenye mahitaji maalumu,”
alisema.
Alisema mojawapo wa kazi za NAPA-T
kwa kushirikiana na LHC ni kutoa elimu na mafunzo ya kutosha kuhusu ugonjwa huu
ikiwemo katika serikali na mitaa na serikali kuu.
Mkurugenzi Mtendaji wa LHC, Dialla
Kassam, alisema wanajivunia kufanya kazi na NAPA-T na kumshukuru mfadhili
kutoka Uingereza, Kevin Baskerville, ambaye ni mtaalamu wa ugonjwa huu wa
usonji, kwa msaada wake kwani amekuwa akija Tanzania mara kwa mara kutoa
mafunzo na elimu kuhusu usonji.
“Kupitia warsha iliyoandaliwa na
LHC mwaka jana, International School of Tanzanyika (IST) ilishirikiana na
Shule ya Msimbazi Mseto ya watoto wenye mahitaji maalumu na watoto
wa Msinbazi Mseto sasa wanaruhusiwa kwenda IST kuogelea matra moja kwa wiki,”
alisema na kuongeza kuwa LHC inafaya kila jitihada kuunganisha shule zenye
mahitaji maalumu na shule za serikali.
Alisema LHC pia imekuwa ikitoa
msaada kwa shule ya watu wenye Usonji ya Mbuyuni kwa kupitia wataalamu wa
kujitolea kutoka pembe zote za dunia na kusimamiwa na LHC ambayo pia hutoa
rasilimali za elimu kwa shule hiyo.
“Kwa msaada wa Kevin, tumeweza
kujenga ushirikaino wa muda mrefu na shule ya watoto wenye mahitaji maalumu
iliyoko uingereza iitwayo Hope School iliyoko Newark ambayo imeahidi kuendelea
kutoa msaada wa vifaa na mafunzo kwa shule ya Msimbazi Mseto ambayo ni ya
serikali,” alisema.
Alisema LHC pia inafanya kazi
kwa karibu na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili hasa kitengo cha watu wenye
matatizo ya akili, ili kutafuta wafadhili ili kuanzisha kituo cha kwaza kabisa
cha watu wenye mahitaji maalumu nchini. Kituo hicho kitakuwa na wataalamu wa
kutosha ambao watakabiliana na matatizo mbalimbali ya kiakili ikiwemo usonji.
Baadhi ya dalili za usonji ni mtoto
kutoweza kumtizama mtu machoni, kutoitika wakati anaitwa, kushindwa
kucheza na watoto wenzake wenye umri sawa, kushindwa kuwasiliana na wenzake,
kukataa kubebwa na kukumbatiwa, kutamani kuwa peke yae muda wote na kushindwa kuonesha
au kuelewa hisia mbalimbali.
Dalili nyingine ni tabia
kubadilikabadilika, kuwa mgomvi, kutopenda mabadiliko, kuchelewa kuzungumza,
kurudiarudia mambo Fulani kama vile kutikisa kichwa, kuchezesha mikono,
kunyatanyata na kuzungukazunguka.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.