Mrisho Ngassa (kushoto) akimtoka mchezaji wa timu pinzani katika moja ya mechi za Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini |
Hiyo, ni siku moja tangu taarifa za kiungo huyo kusitisha mkataba wake wa kuichezea Free States kwa makubaliano huku tetesi zikienea kuwa nyota huyo atarejea kucheza Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo la Ligi Kuu Bara msimu huu.
Ngassa, alisitisha mkataba wa kuendelea kukipiga Sauz kwa kile alichodai kuwa timu hiyo haina malengo ya kutwaa ubingwa zaidi kushiriki kwenye ligi kuu.
Pluijm aliwataja viungo hao washambuliaji kuwa ni Mzambia, Obrey Chirwa, Juma Mahadhi, Simon Msuva na Deus Kaseke ambao anaamini bado wana uwezo mkubwa wa kuichezea timu hiyo kwa muda mrefu kutokana na umri wao.
Aliongeza kuwa, haoni sababu ya kujaza viungo wengi washambuliaji kwenye kikosi chake kutokana na kutokuwa na tatizo katika nafasi hiyo.
“Nimepata taarifa za Ngassa kusitisha mkataba wake wa kuichezea Free States, labda nikwambie tu, ni ngumu kwangu kusajili kiungo mshambuliaji katika kikosi changu kwa hivi sasa, kwani tayari ninao wanne ambao ni vijana wenye uwezo mkubwa wa kucheza.
“Wachezaji wanaocheza nafasi hiyo (ya Ngassa) ni Chirwa, Mahadhi, Kaseke na Msuva, wote ni wazuri. Tofauti na kasi yao ya kushambulia, pia wana uwezo wa kufunga mabao, ni aina ya uchezaji aliyonayo Ngassa,” alisema Pluijm.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.