Kikosi cha Toto African. |
Mfungaji wa bao la pekee kwa Toto African alikuwa, Waziri Junior dakika ya 36 aliyemshinda mbio beki wa Mwadui na kufumua shuti maridhawa lililomshinda kipa wa Mwadui Shahban Kadri na kutinga nyavuni.
Huo unakuwa mwanzo mzuri kwa kocha Rogasian Kaijage aliyechukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa kocha wa timu hiyo John Tegete aliyeondolewa baada ya msimu uliopita kumalizika – na mwanzo mbaya wa kocha wa Mwadui, mwenye tambo na maneno mengi Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.
Kikosi cha Mwadui Fc. |
Mabadiliko ya Toto African ndani ya ungwe ya kipindi cha pili, Frank Sekule (9) anaingia badala ya Hamad Mbumba anayetoka (25), pembeni kushoto anaonekana kocha wa Mwadui Fc Jamhuri Kihwelo. |
Hadi mwisho wa mchezo mashabiki walishuhudia Mwadui Fc wakitoka vichwa chini mara baada ya kukomelewa bao 1-0 dhidi ya Toto African ya Mwanza. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.