Wachezaji wa timu ya moro kids wakishangilia baada ya kunyakua kombe la mashindano ya Airtel Rising Stars kwa kuifunga timu ya Angrikana 1-0 katika uwanja wa Jamhuri Morogoro jana. |
Timu
ya vijana ya Moro Kids imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya vijana chini
ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars baada ya kufanya kazi ya ziada na
kuishinda timu ngumu ya Angrikana 1-0 katika mchezo wenye upinzani mkali
uliochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana.
Goli
hilo la ushindi liliwekwa kimiani na mshambuliaji machachari Nyamawi Juma katika
dakika ya 22 baada ya kuwazidi mbio walinzi wa Angrikana na kuachia shuti kali
lililotinga wavuni. Goli liliibua nderemo na vifijo kutoka kwa mashabiki
waliojitokeza kwa wingi kushangilia timu yao.
Angrikana
walijibu mapigo kwa kufanya mashambulizi mfululizo ambayo hata hivyo hayakuweza
kuzaa matunda. Kipingi cha pili walikianza kwa matumaini ya kupata goli la
kusawazisha lakini hadi dakika ya mwisho matokeo yalibaki kuwa 1-0.
Akikabidhi
kikombe kwa washindi, Meya wa manispaa ya Morogoro Pascal Kihanga ambaye
alikuwa mgeni rasmi aliwapongeza Morogoro Kids kwa mafanikio makubwa na
kuwataka kuendelea kufanya mazoezi kwa kujituma huku wakifuata maelekezo ya
walimu wao. “Kwa kufanya hivyo kutawaweka katika nafasi nzuri ya kutimiza ndoto
zenu za kufanikiwa katika maisha kupitia soka”, alisema.
Aliwataka
viongozi wa soka mkoani Morogoro pamoja na makocha kuhakikisha wanachagua
vijana wenye vipaji ili kuuwakilisha vyema mkoa wa Morogoro kwenye fainali za
taifa za Airtel Rising Stars zinazotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam
kuanzia Septemba 6 hadi to 11.
Wakati
wa mechi hizo za mkoa makocha walipata fursa ya kuwatathimini uwezo wa kila
mchezaji na kuchagua vijana wenye vipaji kuunda kombaini ya mkoa. Mikoa mingine
ambayo tayari imeshaunda vikosi vyake ni kwa fainali hizo ni Ilala, Kinondoni,
Temeke and Mwanza.
Fainali
hizo za kila mwaka itazikutanisha timu za wavulana na wasichana kutoka mikoa ya
kisoka ya Ilala, Kinondoni na Temeke. Washiriki wengine watatoka Mwanza,
Morogoro, Mbeya, Lindi, Arusha na Zanzibar.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.