MABINGWA
watetezi, Yanga SC wameanza vizuri Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
baada ya kushinda mabao 3-0 dhidi ya African Lyon Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Pongezi
kwa wafungaji wa mabao hayo, viungo Deus David Kaseke aliyefungua pazia kipindi cha kwanza, Simon Msuva na Juma Mahadhi.
Katika
mchezo huo uliochezeshwa na refa Rajab Mrope wa Ruvuma, Mirambo
Tshikungu wa Mbeya na Janeth Balama wa Iringa, hadi mapumziko Yanga
walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Bao hilo lilifungwa na Kaseke dakika ya 18, akimalizia pasi ya winga Simon Msuva, ambaye leo alikuwa katika kiwango chake.
Donald Ngoma wa Timu ya Yanga (jezi 11) katikati akijaribu kuwatoka mabeki ya Lyon, kulia ni Abdul Hilary na namba 26 mgongoni ni Amani Peter
Wanachama wa Timu ya Yanga wakimpungia mikono SimonMsuva
Simon Msuva, akiwapungia mikono wanachama na wapenzi waliokuwa wakimpungia mikono katika Uwanja wa Mpira wa Taifa
Mchezo ulianzia hapa kutoka kwa Harun Niyonzima kwa kmpatia pasi Simon Msuva kwa kupachika mpira katika nyavu za goli la Afikan Lyon, angalia picha tatu za chini na kufanikiwa kumtoka Kipa wa Lyon
Simon Msuva wa Timu ya Yanga akiwa katikati akimtoka Omar Salum kushoto na kufanikiwa kumtoka mlinda mlango wa goli la Lyon, Youthe Rostand
Simon Msuva wa Timu ya Yanga akiwa katikati akimtoka, Omar Salum kushoto na kufanikiwa kumtoka mlinda mlango wa goli la Lyon, Youthe Rostand
Simon Msuva wa Timu ya Yanga akiwa kulia akimtoka, Omar Salum na kufanikiwa kumtoka mlinda mlango wa goli la Lyon, Youthe
Rostand, hapa mlinda mlango akishuhudia kwa macho mpira unavyo tinga golini, mpira uliopigwa kwa kicha na Simon Msuva katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam
Simon Msuva kulia akifurahi baada ya kuipatia timu yake goli akiwa na Juma Mahadhi
Donald Ngoma akiwana Mpira
Wanachama wa Timu ya Simba wakiwa na butwaa kutoamini kinacho tokea Uwanjani hapo. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.