MAFUNZO YA MPIRA WA
KIKAPU KWA WATOTO NA VIJANA (CHILDREN& YOUTH BASKETBALL CLINIC) KUFANYIKA
SEPTEMBA KWA KUSHIRIKIANA NA KOCHA GEORGE ELLIS KUTOKA NCHINI MAREKANI HAPA
MKOANI MWANZA.
Chama cha mpira wa kikapu mkoani Mwanza (MRBA) kwa
kushirikiana na Shirikisho la mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Halmashauri ya
Manispaa ya Ilemela(kitengo cha Utamaduni na Michezo) sambamba Planet Social
Development (PSD), tunaandaa mafunzo ya siku moja ya mpira wa kikapu kwa watoto
na vijana kwa kushirikiana na Kocha George Ellis kutoka nchini Marekani siku ya
Jumatatu ya tarehe 12 Septemba 2016.
Mafunzo haya ambayo ni muendelezo wa program ya uibuaji
vipaji na mafunzo yanayoendelea katika kiwanja cha mpira wa kikapu Kiloleli,
yatahusisha pia makocha kutoka Dar es Salaam na Mwanza ikiwa nao ni sehemu
kujifunza namna ya kuendesha mafunzo kama haya kwa watoto na vijana.
Tunatarajia mafunzo haya kufanika katika uwanja wa CCM
Kirumba ama Kiloleli, yatajumuisha wanafunzi wanaocheza mchezo huu kutoka
katika shule mbalimbali za msingi na
sekondari zilizopo hapa jijini Mwanza kwa maana ya Wilaya ya Ilemela na
Nyamagana na pia wachezaji kutoka katika shule mbalimbali.
Coach George Ellis ambae alishawahi kuja hapa Tanzania mwaka
jana 2015 na kuendesha mafunzo mbalimbali akiwa na kocha mkuu wa timu ya Taifa
ya mpira wa kikapu ya Tanzania, Matthew McCollister, anatarajiwa kufanya
mafunzo haya kwa mikoa mitatu kwa kuanza na Dar es salaam, Mwanza na Arusha.
Kwetu sisi tunawaomba wadau mbalimbali wajitokeze kusaidia
kufanikisha mafunzo haya kwa maana ya chakula na malazi kwa Kocha George na
makocha watakaotoka Dar,usafiri wa ndani,
maji ya kunywa kwa washiriki, usafiri wa wachezaji wanaotoka pembezoni,
jezi na tshirts.
Bado tuna imani kupata support kutoka kwa wadau na
makampuni/taasisi mbalimbali ambao tulikuwa nao wakati wa uzinduzi wa program
hii iliyozinduliwa rasmi na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
makazi, Mheshimiwa Angeline Mabula (MB).
Wadau hao ni Mkurugenzi Manispaa ya
Ilemela, CRDB Bank, FNB Bank, The Angeline Foundation, MOIL, Chemi & Cotex
Co. Ltd, PEPSI, Atlas Copco na wadau wengine mbalimbali.
Tuna imani hapo baadae wachezaji wa Mwanza watapata nafasi ya
kwenda kusoma na kucheza nchini Marekeni kwa maana ya Scholarship endapo
watakuwa wanafaulu vizuri katika masomo na kufanya vizuri katika mchezo huu
kwani huendana sambamba. Tunataraji Kocha George ataingia hapa tarehe 11
Septemba 2016.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.