ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, July 31, 2016

MWILI WA SENGA WASAFIRISHWA LEO KWENDA MWANZA KWA MAZISHI.


Dar es Salaam. 
Mwili wa aliyekuwa Mpigapicha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, Joseph Senga (58) umesafirishwa leo kwenda nyumbani kwao, Shushi-Nyambichi, Kwimba mkoani Mwanza kwa ajili ya maziko hapo kesho.
Akizungumza wakati wa kuuga mwili wa marehemu Dar es Salaam mapema leo, msemaji wa familia, Charles Kapama amesema maziko yatafanyika kesho saa nane mchana baada ya mwili kuwasili kijijini.

Viongozi mbalimbali walijumuika na ndugu, jamaa na marafiki wa familia hiyo kuuga mwili wa marehemu Senga ambaye alifariki dunia Julai 27 katika hispitali ya BLK, New Dehli India alikokwenda kupatiwa matibabu, katika uwanja wa mpira uliojirani na nyumbani kwake, Sinza jijini hapa.
Viongozi hao ni pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, Mwenyekiti wa Chadema,  Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika na Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Joseph Senga, aliekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, aliefariki Dunia hivi karibuni, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo, iliyofanyika katika Uwanja wa TP, Sinza Uzuri, Jijini Dar es salaam.
Aliyekuwa mgombea urais kupitia Chadema na Ukawa, Edward Lowassa amekutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Mnauye leo katika jumuiko la kuuaga mwili wa aliyekuwa Mpigapicha wa Tanzania Daima, Joseph Senga.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.