ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, July 31, 2016

PROF JAY KUZINDUA MASHINDANO YA KUCHEZA MUZIKI YA KIMATAIFA.


Mbunge wa mikumi Joseph Haule anatarajia kuzindua mashindano ya kucheza muziki wa kizazi kipya yakiwa na lengo la kupata muwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya dunia yaliyotarajia kufanyika mwezi Agosti mwakani jijini Glassgow nchini Scotchland.

Profesa Jay atafanya uzinduzi huo Agasti 7 mwaka huu katika ukumbi wa Maisha Bassement  jijini Dar es salaam ikiwa ni mashindano ya kitaifa yaliyoandaliwa na Taasisi ya United Dance Organisation East Africa yakitumia jina la Dance Battle Zone.

Professor Jay ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwakilisha jimbo la Mikumi, kupitia sanaa kwa sasa anamiliki wimbo mpya uliokuja kwa mahadhi ya ki-swazi zaidi wimbo unaitwa 'Kazi Kazi'  ambao unatambulisha kipaji chake cha ziada katika muziki kwani kwa miaka sasa amekuwa akihusika na muziki wa Hip Hop, lakini time hii kajikita katika Singeli.
“Kwa hiyo kila mkoa hii UDO East Africa itasajili vijana ambao tutaridhika nao ambao wanavipaji vya ‘ku-break dance’ wapatao 20 kisha watashindana kupata mshindi mmoja ambaye atajishindia zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni moja, tuzo ya UDO na medali ya Dhahabu”

“Zawadi nyingine kwa nafasi ya pili ni medali, na washiriki wengine waliosalia yaani wa tatu hadi wa tano watakwenda kushiriki fainali ya kitaifa ambayo inatarajiwa kufanyika mwezi April mwaka 2017”

Mikoa mingine itakayoshiriki mashindano hayo ni pamoja na Dodoma (Septemba) , Arusha (Oktoba), na Zanzibar (Disemba) ambako kati ya washiriki 20 watakao sajiliwa washindi watano kutoka kila mkoa watashiriki fainali ya Taifa itakayofanyika April mwakani  jijini Dar es salaam.


Aidha mshindi wa kwanza wa kila mkoa atanyakuwa kitita cha shilingi milioni moja. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.