ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, June 27, 2016

AIRTEL YAZINDUA MSIMU MPYA WA 6 WA MICHUANO YA AIRTEL RISING STARS 2016

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano akimuonesha Waziri wa Habari, Utamanduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye  baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys waliopatiakana kupitia michuano ya Airtel Rising Stars wakati wa uzinduzi wa awamu ya sita ya michuano hiyo uliofanyika Dar es Salaam Jumapili Juni 26 2016.
Waziri wa Habari, Utamanduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akipinga mpira kuashiria uzinduzi wa rasmi wa michuano ya Airtel Rising Stars 2016. Uzinduzi huo umefanyika Jumapili 26 Juni 2016 kwenye makao makuu ya Airtel Tanzania Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamanduni ,Sanaa na Michezo Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa michuano ya Airtel Rising Stars 2016 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano akiongea wakati wa uzinduzi wa msimu wa 6 wa Airtel Rising Stars
Rais wa TFF Jamal Malinzi akiongea wakati wa uzinduzi wa msimu wa 6 wa Airtel Rising Stars
Waziri wa Habari, Utamanduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye (katikat) akiwa katika picha ya pamoja na viongezi wa TFF pamoja na Airtel Mara baada ya uzinduzi wa Msimu wa sita wa michuano ya Airtel Rising Stars
Wafanyakazi wa Airtel wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari, Utamanduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye wakati wa uzinduzi wa wa Msimu wa sita wa michuano ya Airtel Rising Stars
 Airtel yazindua msimu wa 6 wa michuano ya Airtel Rising Stars 2016

Dar es Salaam, Jumapili 26 Juni 2016  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Nape Nnauye leo amezindua msimu wa sita wa mashindano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars na kuwapongeza Airtel Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali pamoja na shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) za kukuza mchezo wa soka.

“Programu za soka za vijana ndiyo muhimili wa maendeleo ya soka popote pale duniani. Ndiyo maana nasisitiza umuhimu wa mashindano ya Airtel Rising Stars ambayo matunda yake yameonekana dhahiri katika kipindi cha miaka mitano iliyopita”, alisema Nnauye.   

Alitoa mfano wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys ambayo wachezaji wake 10 wa kutumainiwa wametokana na Airtel Rising Stars. “Matunda ya Airtel Rising Stars vilevile yanaoneka dhahiri kwenye timu ya taifa ya wanawake Twiga Stars ambayo wachezaji wake wote wanatokana na programu hii ya vijana”, alisema Nnauye. Klabu za daraja la kwanza na ligi kuu Tanzania bara pia zinafaidi matunda ya Airtel Risings Stars.

Waziri amewataka viongozi wa soka kusimamia vizuri pragarmu ya Airtel Rising Stars ili kuweza kubaini vipaji vingi zaidi kupitia mashindano haya ya vijana ya kila mwaka yakishirikisha timu za wasichana na wavulana kuanzia ngazi ya mkoa na kuhitimishwa kwa fainali ya Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano alimhakikishia waziri kuwa kampuni ya Airtel Tanzania ina nia thabiti ya kuendelea kudhamini michuano hiyo ambayo imesaidia kuzalisha wachezaji wengi chipukizi hivyo kuendeleza mchezo huo marufu hapa nchini.

Alisema Airtel Rising Stars mwaka inafanyika chini ya mwanvuli wa kampeni ya Airtel RURSA iliyozinduliwa mwaka jana kwa lengo la kuwahamasisha vijana kutumia fursa mbalimbali walizonazo ili kujiendeleza kiuchumi. “Airtel Rising Stars yenyewe ni Airtel FURSA kwa kuwa inawawezesha vijana kutumia vipaji vyao kujikwamua kimaisha kupitia mpira. Mpira ni chano cha kipato cha kuaminika”, alisema.

“Kwa kuwa na wateja wengi nchi nzima Tanzania bara na Zanzibar, Airtel Tanzania tunawiwa kuendelea kutoa sehemu ya faida yetu kwa jamii kupitia mchezo wa mpira wa miguu ambao ni marufu kuliko michezo yote hapa Tanzania. Ni njia ya kuwashukuru wateja wetu kwa kuedelea kutuunga mkono”, alisema.  

Kwa upande wake, Rais wa TFF Jamal Malinzi alisema programu ya Airtel Rising Stars imeleta mapinduzi na kubadilsha kabisa sura ya mchezo wa soka hapa nchini. “Nawapongeza Airtel Tanzania kwa kuendelea kutuunga mkono. Naamini kwamba tutapata mafanikio makubwa zaidi siku za usoni”, alisema.

Airtel Rising Stars mwaka huu itashirkisha timu kutoka mikoa ya Mwanza, Morogoro, Mbeya, Temeke, Ilala, Morogoro (wavulana) wakati mikoa itakayoshirikisha timu za wasichana ni Ilala, Kinondoni, Temeke,  Arusha, Lindi na Zanzibar

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.