Wakati Serikali ya awamu ya Tano ikiendelea kujikita katika juhudi zake za kuisafisha nchi toka wimbi la watenda kazi wabovu, rushwa iliyokithiri na kuwaumbua wezi wa mali Umma waliotapakaa kila kona ya nchi, manyanyaso, ukiukwaji wa haki za binadamu pamoja na dhuluma toka kwa wawekezaji wa kigeni inatajwa kuwa ni jipu jingine sugu linalohitaji mtumbuaji.
Zaidi ya wafanyakazi 300 wa kampuni ya China Communications Contructions Ltd (CCCC), inayojenga yenye urefu wa kilometa 71.8, kuanzia Lamadi hadi Bariadi kwa kiwango cha lami, wamegoma kuingia kazini wakimtaka mwajiri wao kuwalipa mapunjo pamoja na malimbikizo yao ya mishahara ya miaka mitatu na kupinga kitendo cha baadhi yao kufukuzwa kazi kiholela bila kulipwa stahiki zao.
Mgomo huo ulianza majira ya saa kumi na mbili juzi alfajiri, kwa wafanyakazi hao kukusanyika nje ya lango kuu la kuingia ndani ya kambi hiyo ya wakandarasi kutoka China iliyopo katika kijiji cha Nyakabindi wilayani Bariadi.
Baadhi ya wafanyakazi hao wakizungumza kwa hisia, baada ya askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mkoa wa Simiyu kuwasili katika eneo hilo kwa lengo la kuwatawanya walikuwa na haya ya kusema.
Afisa raslimali watu wa kampuni hiyo Rosemary Mayunga, na viongozi wengine wakuu wa kampuni hiyo walipotakiwa kuzungumzia madai ya wafanyakazi hao waliamua kugeuka kuwa mabubu huku wakificha sura zao mbele ya kamera ya mwandishi wetu.
Hata hivyo, mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka amelitolea ufafanuzi suala hilo baada ya kukutana na uongozi wa kampuni hiyo, wawakilishi wa wafanyakazi na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo ofisini kwake.
PICHA ZOTE NA ZEPHANIA MANDIA

Kampuni ya CCC imeamua kuwapunguza watumishi bila barua wala vielelezo vyovyote vya kimaandishi.
PICHA ZOTE NA ZEPHANIA MANDIA
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.