Dkt. Lyatonga Mrema ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na EATV kuhusu miaka 32 ya kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania Edward Moringe Sokoine ambaye alihudumu kwenye awamu ya kwanza ya Mwl. Julius Nyerere ambapo alifariki akiwa na cheo cha waziri mkuu tarehe 12.04.1984 kwa ajali ya gari.
Hapa ndipo alipofia aliyekuwa Waziri Mkuu , Edward Moringe Sokoine , Aprili 12, 1984 akitokea Mkoani Dodoma , eneo hili ni Wami Ruhindo , kilometa 40 kabla ya kufika mjini Moro. |
Kuhusu Mrema kuomba kazi kwa Dkt. Magufuli Mrema amesema kwa kutambua rekodi yake ya utendaji kazi Rais Dkt. Magufuli aliwahimiza wananchi wa Vunjo wamchague kipindi cha kampeni na yeye akampigia kampeni na Rais akawaambia wananchi wa Vunjo kwamba Mrema akikosa ubunge atapangiwa kazi nyingine ndiyo hiyo wananchi wanaulizia.
Aidha Mrema amesema kuna maeneo ambayo yeye anafiti siyo lazima apewe madaraka makubwa mimi sihitaji ukuu wa mkoa au uwaziri anipe kazi yoyote na nikionana naye nitamkonyeza maeneo ambayo ninafiti ili nimsaidie kutumbua majipu.
Hata hivyo Dkt. Mrema amempongeza Dkt. Magufuli kwamba ni mtendaji ambaye ameamua bila kusukumwa kupambana na mafisadi na kwamba yeye ni alfa na omega na kazi hiyo ameonyesha kwamba atafanya vizuri kuliko Sokoine na Mrema.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.