ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, February 10, 2016

WAKAZI WA RUFIJI MKOANI PWANI WAKUMBWA NA MAFURIKO WAKOSA SEHEMU YA KUISHI

NA VICTOR MASANGU, PWANI
WANANCHI  zaidi ya 5000 katika Wilaya ya rufiki Mkaoani Pwani kwa sasa  hawana mahali pakuishi kutokana na nyumba zao kukumbwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali hapa nchini.  

 Kufuatia kutokea kwa mafuriko hayo Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injiania Evarist Ndikilo amekwenda katika eneo la tukio  na kujionea athari zilizojitokeza kwa wananachi hao wa wilyani rufiji kutokana na mvua hizo zilizosaababisha mafuriko.

Akizungumza na wahanga wa mafuriko hayo Ndikio alisema kwamba kutokana na hai hiyo serikali Mkoa wa Pwani imechukua hatua za haraka kuwasaidia wananci hao kwa kutoa chakula cha dharura tani 1283 za mahindi kwa ajili ya wananchi hao.
 
Ndikilo alisema kuwa  mbali na serikali kutoa tani hizo za mahindi pia imetoa mbegu za mahindi tani 10 sambamba na tani 5 za mtama ambazo zinastawi kwa kipindi cha mudamfupi ii wannaachi waweze kuzipanda katika ukanda wa juu ii ziweze kuwasaidia katika upatikanaji wa chakula.

“Kwanza kabisa mimi nawapa pole wale wote ambao wamepata na maafa haya ya mafuriko na wengine kukosa sehemu ya kuishi lakini nataka kuwahakikishia kuwa serikali yenu ipo pamoja nanyi katika kuhakikisha unawasaidia huduma zote muhimu ambazo zinastaili ikiwemo kuwapatia chakula kw ahiyo msiwe na hofu yoyote,”
 
“Lkini ombi langu kubwa kwa kipindi hiki kwa wanaanchi ni kuwa makini sana kwani mvua bado zinaendelea kunyesha na na zimeleta maafa makubwa kama mnavyoona kwa hiyo cha msingi kama kuwa wnanchi bado wanaendelea na shughuli za kulima karibu na mabonde ya mito wasiendelee kulima  katika maeneo hayo kwani wanaweza kusombwa na maji,”alifafanua Ndikilo.

Pia Ndikio aliwaomba wahanga hao wa mafuriko kuhakikisha wanakitumia vizuri chakula amabcho kimetolewa na serikali kwani katika kipindi hiki uende mahitaji ya chakula yakaongezeka zaidi kutokana na mahitaji mwengi ya wananchi wenywe hivyo ni vema kuwa na matumizi mazuri.
 
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwa sasa kazi kubwa inayofanywa na serikali ni kutoa elimu kwa wananachi na kuwahamasisha wale wote waliokumbwa na mafuriko watoke mara moja katika maeneo ya  mashamba kwani ni hatari kwa masiha yao pindi mvua inaponyesha.


Akizungumzia kuhusina na baadhi ya wafanyabiashara amabo wamekuwa na tabia ya kupandisha bei ya vyakula pindi wnapoona maafa kama hayo yamejitokeza waacha mara moja kufanya hivyo kwani ni kwakandamiza wananchi.

 " Wafanyabiashara wasiowaungwana wasitumie janga hili kujinufaisha kwa kupandisha bei ya vyakula, kwa kutambua hilo tumewapa vibali wafanyabishara 6 wenye uwezo ili wanunue  tan 10 za mahindi na kusaga unga na kuwauzia wananchi kwa bei nafuu kwa jimbo la kibiti na ikwiriri," alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Rufiji Nurdin Babu aibainisha kuwa kutoka ana mvua hizo zinazoendelea kunyesha tayari jumla ya hekta 8138.4 za mpunga na tani 7171.2 za mahindi zimeathirika na maji na kuwa mazao hayo yalikuwa katika hatua za mwisho kwa ajii ya kuvunwa.

Babu aliongeza mafuriko  yaliyotokea katika wilaya yake  yalianza tangu  juzi usiku na kuvikumba vijiji mbali mbali ikiwemo kijiji cha uwe na mhoro na kusababisha daraja la muhoro kuvunjika na hivyo wananchi kuvuka kwa kutumia mitumbwi pamoja na  boti.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.