ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, February 29, 2016

TATIZO LA DAMU SALAMA WILAYANI KWIMBA SASA LAPATA UFUMBUZI.

Mbunge wa Kwimba Mhe. Mansour akimkabidhi jokofu la kuhifadhia damu salama Kaimu Mganga Mkuu Dr. Michael na kumsisitiza kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi wajitokeze katika kuchangia damu suala ambalo limekuwa changamoto kubwa sana nchini kupitia upungufu uliopo.
Sehemu ya makabidhiano.
Ili kufikia malengo yaliyokusudiwa yaani kuokoa maisha ya wananchi kwenye hospitali hiyo, Mbunge wa Kwimba Mhe. Mansour akisisitiza jambo kwa Mkuu wa wilaya hiyo Bi. Pili Moshi na Kaimu Mganga Mkuu Dr. Michael.
Mbunge wa Kwimba Mhe. Mansour, hapa akiteta na Kaimu Mganga Mkuu Dr. Michael kwa masuala mengineyo yaliyo sugu kama sehemu ya changamoto kuhakikisha kwamba masuala yote ya msingi yanayotatulika yanapatiwa ufumbuzi wa haraka.
Jokofu lililotolewa lina thamani ya shilingi milioni kumi na nane.
PICHA ZOTE NA ZEPHANIA MANDIA WA GSENGO  BLOG.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.