ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 16, 2015

MSHINDI WA AIRTEL TRACE MUSIC STARS SAFARINI KUREKODI NA AKON

Mshindi wa Airtel Trace Music Stars, Mayunga Nalimi akiongea na waandishi (hawapo pichani) wakati wa tukio la kumuaga kwa ajili ya kwenda kurekodi video ya mziki na kupata mafunzo toka kwa mwanamuziki wa kimataifa Akon nchini Marekani. hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika katika makao makuu ya ofisi ya Airtel Morocco jijini Dar Es Salaam. Pichani katikati ni Afisa uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde, akifatiwa na Mwalimu wa sauti Tony Joet.

MSHINDI wa shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika, ameondoka nchini Jana kuelekea nchini Marekani kwa lengo la kupata mafunzo na kurekodi wimbo wake.

Nalimi Mayunga ameondoka jana Jumatatu usiku na kwenda kufanya kazi na nguli wa mzuki wa R&B nchini Marekani Bwana Akon ambapo anatarajiwa kukaa muda wa wiki moja kisha kurejea nyumbani tarehe 24 Novemba. 

Akiongea wakati halfa ya kumuaga, Afisa habari mwandamizi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Aristide Kwizera alisema” Tunajisikia furaha kuona vijana wa kitanzania wakitangaza sanaa na nchi yetu duaniani kupitia muziki.

Napenda kumpongeza sana mayunga kwa kupata ushindi ambao umempatia nafasi hii nono na kumwomba atumie vyema fursa hii. Sisi kama wadau wakuu wa sanaa nchini tunawapongeza sana Airtel kwa kuanzisha program zenye lengo la kukuza sanaa na muziki wa nchini kama hii ya Airtel Trace Music Stars na nyingine nyingi. 

Afisa uhusiano na mwandamizi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Aristed Kwizera (kushoto) akimuaga mshindi wa Airtel Trace Music Stars, Mayunga Nalimi kwa ajili ya kwenda kurekodi mziki na kupata mafunzo toka kwa mwanamuziki wa kimataifa Akon nchini Marekani , katika hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika katika makao makuu ya ofisi ya Airtel Morocco jijini Dar Es Salaam. Anayeshuhudia (katikati),ni Afisa uhusiano wa Airtel Tanzania jane matinde .
Naye mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga alisema” ile siku niliyokuwa naisibiria kwa hama leo imefika na nimejipanga kuondoka kwenda kujifunza mengi na ya msingi katika maisha yangu ya muziki . 

Naamii safari hii itakuwa ni ya mafanikio makubwa na mwanzo wa hatua yangu ya mafanikia katika tasinia ya muziki Napenda kuwaambia watanzania wajiandae kusikia kibao na video kali ntakayoifanya na Akon kwani nimejiandaa vya kutosha kuhakikisha nashirikiana nae vyema ili tunatoa nyimbo kali itakayowapa burdani wapenzi wa muziki pande zote duniani. 

Aliongeza Mayunga Kwa upande wake Aliyekuwa jaji katika shindano la Airtel Trace Music Stars Tanzania na Mwalimu wa Muziki Tony Joet alisema” mayunga amekuwa akifanya mazoezi kujiandaa kwa deli hii toka alipotangazwa mshindi wa Airtel Trace Afrika. 

Ninaimani naye kwani ameonyesha uwezo mkubwa na nidhamu ya hali ya juu na naamini atafika mbali na namtakia kila laheri katika safari yake” Akiongea kwa niaba ya Airtel Afisa Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde alisema” mipango yote ya safari imekamilika na mayunga atakuwa marekani kwa muda wa wiki moja, tunaamini mayunga atakaporejea atakuwa tofauti kabisa na alivyokwenda na ndio hasa lengo letu sisi Airtel, kuwawezesha na kuwainua vijana kubadilisha maisha na kufikia malengo yao. 

Shindano la muzuki la Airtel Trace Music stars lilizinduliwa octoba 2014 na huu ndio msimu wa kwanza wa shindano hili ambalo limewapatia vijana watanzania na waafrika nafasi ya kuonyesha vipaji vyao na kupata fulsa mbalimbali za muziki.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.