ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 16, 2015

NDUGAI USO KWA USO NA GOLE MEDEYE,RICHARD LYMO, HASHIM RUNGWE,NA ROBERT KISININI KINYANG'ANYIRO CHA USPIKA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BAADA ya wagombea wawili waliopitishwa kugombea nafasi ya Uspika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kupitia CCM, Abdula Mwinyi na Dr. Tulia Ackson Mwansasu kujitoa Kamati Kuu ya chama hicho imempitisha Job Ndugai kuwa mgombea nafasi ya Uspika ambapo atakutana na mgombea aliyesimamishwa na Umoja wa Vyama vinavyounda UKAWA.


Umoja wa vyama vinavyounda UKAWA wao wamemsimamisha Goodluck Ole Medeye kugombea nafasi ya Uspika na Bi. Magdalena Sakaya kwa nafasi ya Naibu spika wa Bunge akitegewa kuleta ushindani mkali kwenye kinyang'anyiro hicho dhidi ya Dr. Tulia Ackson Mwansasu wa CCM ambaye mara baada ya kujiengua nafasi ya juu ya Uspika amechukuwa fomu upande wa Naibu spika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Majina ya wagombea toka vyama vingine katikanafasi ya Uspika ni kama ifuatavyo:-

-Richard Lymo (TLP)
-Hashimu Rungwe (CHAUMA)
-Robert Kisinini (DP)

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.