WIKI moja baada ya kutengamaa kwa mashine ya uchunguzi wa magonjwa ya MRI (Magnetic Resonance Imaging), Hospitali ya Taifa Muhimbili imesitisha kutoa huduma hiyo jleo kutokana na kuharibika kwa kifaa kimojawapo huku mashine ya CT Scan ambayo ni muhimu zaidi ikiwa bado haijatengamaa.
Awali mashine hizo ambazo zilisimamisha huduma ya uchunguzi kwa muda wa miezi miwili kabla ya matengenezo, MRI ilianza kufanya kazi baada ya Rais John Pombe Magufuli kufanya ziara ya kushtukiza hospitalini hapo na kuagiza zitengenezwe mara moja.
Akizungumza leo hospitalini hapo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja, Aminiel Buberwa Aligaesha alisema, uongozi umesitisha huduma ya vipimo vitokanavyo na MRI baada ya kuwahudumia wagonjwa 21 kutokana na kifaa kinachoitwa ‘RF Amplifier’ kuharibika.
Akifafanua hali halisi ya mashine hiyo alisema, ilianza kufanya kazi Novemba 11 kwa muda wa siku mbili na ilipofika Novemba 13 majira ya mchana ilionekana kuwa na hitilafu ya kiufundi ambayo inahitaji matengenezo zaidi hali iliyowalazimu kusimamisha huduma hiyo.
Alisema uongozi wa hospitali hiyo umewasiliana na kampuni ya Philips ambayo ina mkataba wa kufanya matengenezo ya mashine za MRI na CT Scan ili kurekebisha hizo hitilafu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.