Press Release Airtel
Tanzania yazindua kadi ya malipo ya 'Airtel Money Tap Tap' • Airtel yawa kampuni ya kwanza kutoa huduma ya kufanya malipo kwa kupitia kadi inayouunganishwa na akaunti ya Airtel Money ya mteja
Dar es Salaam, Jumatatu 12 Octoba 2015, Airtel Tanzania leo imezindua huduma ya kwanza , ya kipekee na kibunifu yenye technologia ya kisasa ijulikanayo kama “Tap Tap” itakayomuwezesha mtumiaji wa huduma ya Airtel Money kufanya malipo kwa njia rahisi na,salama kupitia kadi hiyo Huduma hii itawewazesha wateja na jamii kwa ujumla kutumia maendeleo ya technologia kuleta urahisi katika kuendesha maisha yao.
“Tap Tap” itawawezesha wateja wa Airtel Money kufanya miamala kwa haraka na urahisi kwa kugusisha kadi zao ambazo zimeunganishwa na akaunti ya Airtel money wakati wowote wanapotaka kulipia huduma mbalimbali.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema” Leo kwa mara nyingine tena Airtel tunachua hatua thabiti katika kuboresha maisha ya mamilioni ya wateja wetu kupitia uzinduzi wa huduma hii ya Tap Tap.
Kadi hii ni rahisi kutumia, ili kufanya malipo mteja atagusisha kadi yake kwenye kifaa cha muuzaji na moja kwa moja kufanya malipo kwa kuweka namba yako ya siri, wateja wetu wataweza kulipia huduma mbalimbali katika vituo vya mafuta , maduka ya dawa, baa, saloni, maduka ya rejareja, wataweza kununua muda wa maongezi kwa mawakala wa Airtel Money.
Kupitia kadi hii tunawawezesha watanzania kuwa na usalama na pesa zao na kuondoa haja ya mteja kutembea na pesa wakati wote. vilevile Mteja atakapopoteza au kuibiwa kadi hela zake zitakuwa bado ni salama” Aliongeza kwa kusema , huduma ya “Tap Tap” inadhihirisha dhamira yetu ya kuboresha matumizi ya huduma za kifedha kupitia simu za mkononi na kutengeneza njia mpya ya kufanya malipo katika technologia ya simu za mkononi na kuwaondolea wateja wetu athari zitakazowapata kwa kutembea na pesa nyingi mfukoni “ Tunaamini technologia hii mpya katika huduma za kifedha kupitia simu za mkononi italeta njia mbadala wa kufanya malipo na pia kusaidia katika kuendelea kukuza na kutanua huduma za kifedha nchini.”.
“Ni matumaini yetu kuwa wakazi katika maeneo ya Mbagala, Temeke, Tandika, Ubungo ambapo huduma hii imezinduliwa kwaoleo watafurahia faida zinazotokana na huduma hii ikiwa ni pamoja na kuboresha maisha yao kupita technologia hii ya kisasa” aliongeza Matinde
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.