CHANZO:ISSA MICHUZI
Diamond Platnumz akiwa na moja ya tuzo alizoshinda pamoja na mchekeshaji kutoka Nigeria Basketmouth.
Ommy Dimpoz |
Tuzo tatu alizoshinda Diamond Platnumz. |
Inaweza ikawa siyo mara ya kwanza kwa msanii Diamond Platnumz kuchukua tuzo mbalimbali za kimataifa lakini kwa Vanessa Mdee inaweza ikawa moja kati ya historia nzuri kwake huku Ommy Dimpoz akiwa na kila sababu ya kufurahia tuzo yake ya kwanza ya kimataifa baada ya kujinyakulia tuzo maarufu za Afrimma.
Wasanii hao walijinyakulia tuzo hizo usiku wa kuamkia leo huko Dallas, Marekani ambapo Diamond alichukua tuzo tatu katika vipengele vya Best Dance Video kupitia wimbo wake wa Nana, Best Male East Africa Artist na Artist of The Year huku wimbo wa Alive alioshirikiana na Brackets ukichukua tuzo ya Best Inspirational Song of The Year.
Wakati huohuo mwanadada, Vanessa Mdee akichukua tuzo ya Best Female East Africa huku Ommy Dimpoz akichukua tuzo ya Best New Comer na kufanya Tanzania kukusanya jumla ya tuzo tano.
Washindi wengine wa tuzo hizo katika vipengele tofautitofauti kutoka nchi mbalimbali ni kama vile; God Father, AKA, Yemi Alade, Davido, Wizkid na Yuri.
Hii ni orodha ya washindi.
Best Male (South Africa) – AKA
Best Male (East Africa) – Diamond Platnumz
Best Male (Central Africa) – Yuri Da Cunha
Best Male (West Africa) – Davido
Best Female (East Africa) – Vanessa Mdee
Best Female (West Africa) – Yemi Alade
AFRIMMA Inspirational Song – Bracket feat. Tiwa Savage and Diamond Platnumz for ‘Alive’
Best DJ (US) – DJ Simplesimon
Best Newcomer – Ommy Dimpoz
Best Collaboration – AKA feat. Da Les and Burna Boy for ‘All Eyes on Me’
Best Dance Video – Diamond Platnumz for ‘Nana’
Best Video – Wizkid for ‘Ojuelegba’
Artist of the Year – Diamond Platnumz
Legendary Award – Yossou N’Dou
Na wakati huo huo.....
BASATA LAWAPONGEZA WASANII DIAMOND, VANESSA MDEE NA OMMY DIMPOZ KWA KUSHINDA TUZO ZA AFRIMMA
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) likiwa ni msimamizi na mratibu wa sekta ya Sanaa nchini linapenda kutoa pongezi za dhati kwa Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Nassib Abdul maarufu kama Diamond, Omary Faraji Nyembo maarufu kwa jina la Ommy Dimpoz na Vanessa Mdee maarufu kwa jina la Vee Money kwa kushinda tuzo mbalimbali kwenye Tuzo za African Music Magazine Awards (AFRIMMA) zilizofanyika jijini Dallas nchini Marekani.
Katika tuzo hizo Msanii Diamond ameshinda tuzo tatu ambazo ni Video Bora ya Kucheza (Best Dance Video), Msanii Bora wa Mwaka (Best Artist of the Year) na Msanii Bora wa Kiume wa Afrika Mashariki (Best Male East African Artist). Aidha Ommy Dimpoz na Vanessa Mdee wameshinda tuzo za Best New Artist in Africa (Msanii Bora Mpya Africa) na Msanii Bora wa kike wa Afrika Mashariki (Best Female East African Artist) sawia.
Kuteuliwa kwa wasanii wetu na baadaye kushinda katika tuzo mbalimbali za Afrika na duniani ni ishara kwamba wasanii wetu wanakubalika ndani na nje ya Tanzania na kwamba hawana budi kuhakikisha wanatumia fursa hizi katika kupanua wigo wa fursa za masoko kitaifa na kimataifa.
Baraza linatoa wito kwa wasanii na wadau wote wa muziki kuzidisha ubunifu, nidhamu, bidii, mshikamano na weledi katika kazi wanazozifanya ili wasanii wengi wa Tanzania waweze kuchomoza katika tuzo na majukwaa mbalimbali ya kimataifa kwa lengo la kulitangaza Taifa na kukuza soko la kazi zao.
Ni matumaini ya Baraza kwamba wasanii wataendelea kutambua umuhimu wa kufanya kazi na mapromota wenye upeo na mapenzi mema, kufuata Sheria, Kanuni na taratibu za kutambuliwa na Serikali na zaidi kuhakikisha wanapokwenda nje ya nchi wanafuata taratibu zote sambamba na kukabidhiwa bendera ya Taifa kama ishara ya uwakilishi wa Taifa letu.
SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI
Godfrey Mngereza
KAIMU KATIBU MTENDAJI
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.