ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, September 8, 2015

WANANCHI MSICHAGUE RAIS, WABUNGE NA MADIWANI KWA USHABIKI

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Anthony Dialo (kulia) akiwaomba wananchi wamchague Angelina Mabula mgombea Ubunge kwa Jimbo la Ilemela ifikapo Oktoba 25 mwaka huu kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni Jimbo la Ilemela uliofanyika Kata ya Busweru.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Ilemela katika Kata ya Busweru kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za jimbo hilo kuwanadi, Agelina Mabula (Ubunge) na Madiwani wa Kata 19 za jimbo hilo, kuwaomba wawachague ikiwa ni pamoja na mgombea Urais Dk John Magufuli. 

Na PETER FABIAN, MWANZA.

KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu, amewataka wananchi wa Jimbo la Wilaya ya Ilemela na Kata za Mabatini na Mkuyuni na Butimba Jimbo la Wilaya ya Nyamagana kuwasikiliza wagombea wa vyama vyote ili kufanya uamuzi sahihi katika kuwachagua wagombea Urais, Ubunge na Udiwani badala ya kuwachagua kwa ushabiki.

Mtaturu akiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za Ubunge na udiwani jimbo la Ilemela zilizofanyika katika viwanja vya Busweru shule ya msingi juzi, aliwataka wananchi wa jimbo hilo kutorudia makosa ya kumchagua Mbunge Haighness Kiwia (CHADEMA) kutokana na kushindwa kuwa mwakilishi mwenye dhamira ya kweli kuwaletea maendeleo na kusababisha kubaki nyuma.

Mtaturu alisema kwamba katika uchaguzi wa mwaka 2010 wananchi wa jimbo la Ilemela walifanya ushabiki na kumchagua mtu ambaye ameshindwa kushughulikia kero mbalimbali na kuasababisha jimbo hilo kubaki nyuma kimaendeleo kutokana na miaka mitano ya Mbunge Kiwia na Madiwani wa CHADEMA kupigania posho kwenye vikao vya maamuzi katika Halmashauri ya Manispaa.

“Wananchi kwa hili mlipiga kura za hasira na kuchagua kwa ushabiki lakini hata ninyi ni mashahidi kuwa Mbunge Kiwia ameshindwa kuwaletea maendeleo kutokana na kutumia miaka mitano kufanya shughuli zake binafsi tena nje ya jimbo hivyo mwaka huu mchague wagombea wa CCM kwa na fasi ya Urais, Ubunge na Udiwani kutokana na kuwa na ofisi na anwani inayoeleweka,”alisema.

Katibu huyo aliwataka wananchi watakao hudhulia mikutano ya kampeni ya mgombea wa Kiwia (CHADEMA) kumuhoji Mbunge huyo aliyemaliza muda wake na kutaka tena lidhaa ya kuomba kuchaguliwa tena juu ya fedha za Mfuko wa Jimbo zimefanya shughuli gani ambayo haionekani hata machoni mwenu na kisha awaeleze amefana nini kwa miaka mitano ?,” alisisitiza.

Aidha aliwataka wananchi kuwa makini na kumchagua mgombea Ubunge wa Jimbo la Ilemela kwa tiketi ya chama hicho, Agelina Mabula, mgombea Urais Dk John Magufuli kuwa Rais wa Awamu ya tano na Madiwani wote kutoka Kata 19 kuwa wawakilishi wao watakaosimamia utekelezwaji wa Ilani ya 2015/2020 kwa vitendo na kuwaacha wanaotaka kujinufaisha binafisi kwa kutumia ngazi ya wananchi.

"Wananchi wa Nyamagana muulizeni Wenje kwa miaka yake mitano amefanya nini na wapi msikimbilie tu kusikiliza porojo zake majukwaani, pili muuzizeni fedha za Mfuko wa Jimbo lake amezifanyia nini na pia lazima awaeleze fedha kiasi cha Sh milioni 75 za harambee na Mfuko wa Nyamagana Eductation Foundation (Mfuko wa kusaidia Elimu) zimefanya nini na Kiwia Ilemela mumuulize amefanya nini ila naamini huyo tayari aanze kuaga siyo kufanya kampeni,"alisema

Akiwahutubia wananchi kwa nyakati tofauti katika Kata za Isamilo, Buhongwa, Mabatini na Mkuyuni akimnadi mgombea Ubunge wa CCM jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula ambaye alikuwa Meya wa Jiji la Mwanza aliyemaliza muda wake, Madiwani walioteuliwa na CCM katika Kata hizo na kumwombea kura mgombea Urais Dk John Magufuli wachaguliwe Oktoba 25 mwaka huu.

Mtaturu amewataka wananchi kuachana na watu na wanasiasa wanaofanya maigizo ya kutaka wachaguliwe kuwa wawakilishi huku wakionekana kushindwa kuwa wawakilishi wa kuwasaidia wananchi katika kwawaletea maendeleo na kutatua kero zao katika nafasi ya Ubunge na Udiwani pamoja na wananchi kufanya mabadiliko mwaka 2010 kwa kuwachagua wakiamini wangeweza.

“Mmekuwa na unyonge kwa miaka mitano kwa kuwa na Mbunge Ezekiel Wenje (CHADEMA) wa matukio na akitumia miaka mitano kufanya mikutano ya siasa kila alipowaalika na kushindwa hata kuwahamasisha kuchangia maendeleo na kutafutia ufumbuzi kero na matatizo yenu wananchi ikiwemo kwenye maeneo yenu na yale yaliyohitaji ushirikishwaji wa wananchi kwa ujumla,”alisema.

Mtaturu aliwataka wananchi hao kuwachagua madiwani wa CCM, lakini wamchague mgombea wa CCM,  Mabula kuwa Mbunge kwa kuwa tayari ameweka bayana vipaumbele vyake ambavyo amewatajia kuwa ni Afya, Elimu, Ujasiliamali na Uchumi, Ardhi, Miundombinu ya barabara za Lami, Mawe na Changalawe na Michezo na Sanaa ambayo anayo huakika wa kuyasimamia kwa uhakika akiongozwa na Ilani ya 2015/2020.

Aidha amewataka wananchi kuwa makini kutokana na kuwepo poropoganda zinazofanywa na watu na wanasiasa ambao ni waupinzani wakiwemo UKAWA kuwachafua wagombea wa CCM kuanzia ngazi ya Urais, Ubunge na Udiwani pamoja na kuwatisha kuwa siku ya kupiga kura kutakuwa na vurugu hivyo wapuuzeni na mtunze shahada na Oktoba 25 mwaka huu mchague wagombea wa CCM.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.