NA PETER FABIAN, MWANZA.
MGOMBEA wa Ubunge wa Jimbo la Nyamagana kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stanslaus Mabula, amewataka wananchi wa Kata mpya ya Mabatini kumuchagua aweze kukamilisha ujenzi wa majengo mawili ya vyumba vya mama na mtoto na wanaume katika Zahanati iliyopo ili kufikia kiwango cha kuwa kituo cha Afya.
Mabula akizungumza na mamia ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza katika mukutano wake wa kuomba kura Katani humo juzi katika viwanja vya Kabengwe, alisema kwamba wakimuchagua atahakikisha anasimamia kikamilifu ujenzi wa majengo hayo ili kuwezesha Zahanati hiyo kupandishwa hadhi kuwa kituo cha Afya na kusaidia wananchi kupata huduma ya matibabu wakati wote ikiwemo kulazwa.
Mabula aliweeleza wananchi hao kuwa akiwa Meya wa Jiji la Mwanza kwa kipindi cha miaka mitatu ya 2012 hadi 2015 amewezesha kuwekwa kuikamilisha zahanati hiyo kwa kuhakikisha Halmashauri inapeleka fedha za ukamilishaji wa masuala yaliyokuwa yamebakia na kuachwa na aliyekuwa Diwani wa wakati huo Ezekiel Bahebe (CCM) kabla ya kuangushwa 2010 na Diwani aliyemaliza muda wake, Hassan Kijuu (CHADEMA).
“Naombeni michagulie Bahebe ili awe diwani na mnichague kuwa Mbunge na kura zikae vizuri mpigie pia mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli ili kutekeleza Ilani kwa vitendo na vipaumbele vyangu kwani yapo mambo yatakayotekelezwa na Halmashauri na mengine ntasimamia na kuyatekeleza kama Mbunge na yapo ya serikali kuu yatakayofanywa na Rais na wetendaji wake wa Wizara,”alisema.
Aidha aliwahakikishia wananchi kuwa hata kuwa mtu wa kujifunza kushughulikia vipaumbele kwa kuwa kazi hiyo alikwisha ianza akiwa Meya na sasa ataifanya kwa uhakika akichaguliwa kuwa Mbunge atashughulika kero na changamoto zilizopo katika sekta za Elimu, Miundombinu ya barabara za lami na mawe katani humo, wananchi kupata huduma safi ya maji safi, umeme na kushughulikia kero ya Ardhi huku sekta ya Michezo na Sanaa pamoja na Ujasliamali na Uchumi ili ilenge kutoa ajira na kuleta maendeleo.
Akiwa Katika Kata ya Mkuyuni jana Mabula aliwahakikishia wananchi waliofurika kwenye mkutano katika viwanja vya Sokoni, akiahidi kuwaletea maendeleo kwa kusimamia na kupigania kuhakikisha soko la kimataifa linajengwa katika eneo la Mwalo Mkuyuni na kusaidia wakulima, wavuvi na wafanyabiashara kujipatia sehemu ya kuuzia biashara yao kutokana na kuwepo mipango aliyoiacha.
Mabula alisema akiwa Meya wa Jiji la Mwanza, tayari kulikuwa na mkakati wa kujenga kitegauchumi (soko) kubwa la kimataif`1`a ili kuwezesha jimbo hilo na Halmashauri yake kuwa na chanzo kikubwa cha mapato na wafanyabiashara (machinga), wavuvi na wakulima kuwa na uhakika wa soko pamoja na kutekeleza majukumu yao wakiwa katika eneo la uhakika tofauti na sasa.
“Nichagulieni Donatha Gapi (CCM) kuwa diwani wa Kata hii na mimi mnipigie kura nyingi ili niwe Mbunge wenu lakini kura za Urais mumpingie Dk John Magufuli ili awe Rais wa Awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kukifanya hivyo hakika itaturahisishia kuitekeleza Ilani kwa vitendo katika sekta zote na kukuza uchumi na kipato cha wananchi kwa maendeleo ikiwemo jengo la soku kuu la mjini kati litakalochukua wamachinga, mama lishe na wafanyabiashara wa nafaka, bongambonga na matunda,”alisema.
Kwa upande wake Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Elias Mpanda, amewataka wanawake na wazee kutunza shahada zao za kupigia kura kwa umakini kutokana na kuwepo taarifa za vijana wao wasiokiunga mkono kuweka mkakati wa kuwaibia ili siku ya kupiga kura wasiweze kujitokeza, lakini pia kuwazuia jambo ambalo amewataka wasiwe na wasiwasi na wajitokeze kuwachagua wagombea wa CCM Oktoba 25 mwaka huu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.