ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, September 17, 2015

MARCIANO FASHION DASH KUTIMUA VUMBI REGENCY PARK HOTEL 26, SPT 2015

MARCIANO FASHION DASH KUTIMUA VUMBI REGENCY PARK HOTEL 26, SPT 2015

Saleem Siwila ni mmoja kati ya wadada wenye vipaji vya ku-design mitindo mbalimbali ya mavazi hapa home Tz, ambaye ameona ni vyema kukuandalia Show ili uweze ku-enjoy na wanamitindo kwa pamoja. Hivyo ukiwa kama shabiki wa ukweli unaependa Fashion, basi hii ni habari njema kutoka kwa mwanadada huyo maarufu kwa jina la Saleem Siwila coz anakuletea Fashion Show inayoitwa ‘Marciano Fashion Dash’ itakayo fanyika ndani Regency Park Hotel, chini ya usimamizi wa ‘Hasleem Fashion Design’ 26, September 2015.

Siku hiyo kutakuwa na wanamitindo wengi watakao show love na kuusindikiza usiku huo, kama Asya Idarous, Walter Di Marian, Kulwa Mkwandule, Benja Perfect, Benny Masai kutoka Urban Masai Cllection nk. Unaweza kuingia ni kwa mtonyo wa buku 15,000 tu! na 30,000 tu! kwa (VIP) unakosaje hii! (jichange) tuka-enjoy pamoja.

Burudani ya muziki itakuwepo kutoka kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka hapa Tanzania maarufu kama Baby J, Gigy Money pamoja na Unit X. Mbali na hiyo kutakutana live na Zamaradi Mketema kutoka Clouds, Dida wa Times FM bila ya kusahau Team ya Chanel Ten na Lotus Kyamba & Deo kutoka EATV ( Nirvana) kutakuwa na Red Carpet kali kwa ajili ya watu na pamba zao

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.