ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, September 9, 2015

AIRTEL YANG'ARA KATIKA MAONYESHO YA BIASHARA AFRIKA MASHARIKI

Katibu Mkuu wa Wizara ya viwanda na Biashara Uledi Abbas Musa ( Kushoto) akimkabithi kikombe Afisa masoko na biashara wa Airtel , Emmanuel Raphael mara baada ya kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kuibuka mshindi wa pili katika maonyesho ya Biashara ya Afrika Mashariki ya mwaka huu.

Katika maonyesho hayo Airtel ilipata makombe manne katika vipengele mbalimbali ikiwemo, Mtoa huduma bora , Mtoa huduma bora katika sekta ya mawasiliano, ubora katika mawasiliano ya habari na tecknologia pamoja na mshindi wa pili wa maonyesho kwa mwaka huu. Akishuhudia (katikati) ni mwenyekiti wa Tanzania Chamber of Commerce , Industrial and Agriculture Elibariki Mmari
Afisa masoko na biashara wa Airtel, Emmanuel Raphael katika picha na makombe mara baada ya kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kuibuka washindi katika vipengele mbalimbali katika maonyesho Biashara ya Afrika Mashariki ya mwaka huu.
wafanyakazi wa Airtel kwa pamoja wakiwa na makombe yao mara baada ya kukabithiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya viwanda na Biashara Uledi Abbas Musa mara baada ya kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kuibuka washindi katika vipengele mbalimbali katika maonyesho Biashara ya Afrika Mashariki ya mwaka huu 
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel imepokea vikombe vinne katika maonyesho ya Biashara ya Afrika Mashariki kufatia ubora wake katika kutoa huduma na bidhaa za kibunifu kwa wateja wake. Maonyesho haya ya Biashara ya Afrika Mashariki ni maarufu kwa kuonyesha aina mbalimbali za bidhaa ikiwemo bidhaa za matumizi ya kawaida na ya viwanda, huduma, mashine na teknologia. 

Na maonyesho haya yametoa fulsa ya kukutanisha wadau pamoja na kubadilishana uzoefu wa kibiashara na kuwawezesha ushirikiano wa biashara katika nchini za ukanda wa mashariki. 

Akiongea wakati wa halfa hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Uledi Abbas Musa alisema” Maonyesho haya yana lengo la kuwapatia makampuni yaliyoko katika ukanda wa Afrika ya Mashariki fulsa ya kujitangaza na kukuza biashara zao lakini pia kuwapatia nafasi ya kuboresha mahusiano ya kudumu na wateja wao.

Leo najisikia furaha kuwazawadia kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kuonyesha ubora wake katika huduma, bidhaa, tecknologia za kibunifu na kwa kuwa washindi wapili katika maonyesho ya mwaka huu” Aliongeza kwa kusema” Airtel imedhihirisha dhamira yake ya kutoa huduma za kibunifu na za uhakika za mawasiliano ya simu za mkononi na kutokana na hilo tumeona ni muhimu kuwapongeza na kuwazawadia kwa jitihada zao” 

Kwa upande wake Afisa Masoko na bidhaa wa Airtel , Bwana Emmanuel Raphael alisema” huu ni mwaka watano mfululizo sasa kwa Airtel kushiriki katika maonyesho haya tukuwa na lengo la kufikia wateja wetu , kutoa elimu ya huduma na bidhaa tunazotoa pamoja na kuboresha mahusiano nao. 

Maonyesho haya pia yamekuwa ni fulsa muhimu kwetu kuonyesha bidhaa na huduma zetu za kibunifu na za kisasa na pia ni nafasi pekee ya kushikiana na makampuni mengine yanayoshiriki kila mwaka”

“Napenda kuwashukuru waandaaji wa maonyesho haya kwa kutambua na kuona mchango wetu na tunahaidi kuendelea na dhamira yetu ya kutoa huduma bora na za kibunifu zinazokidhi mahitaji ya wateja wetu.” Aliongeza Raphael Katika halfa hiyo, Airtel ilipokea makombe manne ya ubora katika vipengele vya namba moja kwenye kutoa huduma, namba moja katika sekta ya mawasiliano, namba moja katika teknologia ya mawasiliano ya habari na namba mbili katika maonyesho ya mwaka huu.

Nchi zilizo shiriki katika maonyesho ya mwaka huu ni pamoja na Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda and Burundi

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.