ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, September 9, 2015

MCHANGO WAKO UNAHITAJIKA KUWANUSURU WATOTO WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU.

TANGAZO.

Jumuiya ya Maendeleo ya Watoto Yatima (JUMAC) Kwa kushirikiana na Chama Cha Albinism (TAS) Mkoa wa Mwanza  imeandaa Chakula cha hisani  ili kukusanya fedha na vifaa vya kukamilisha ujenzi wa shule na Zahanati katika kituo cha watoto walio katika mazingira magumu na hatarishi wakiwemo yatima na wenye albinism.
Shughuli hii itafanyika siku ya ijumaa tarehe 11 Septemba 2015  kuanzia saa 1:00 jioni katika ukumbi wa Nyerere, Gold Crest  Hotel jijini Mwanza.
Ili kufanikisha hili Uongozi wa JUMAC kushirikiana na Chama cha Albinism Mkoa wa Mwanza (TAS) Unawaalika wadau wa sekta binafsi ,viongozi na wafanyakazi wa asasi za kiraia na za kiserikali wenye nia kujumuika pamoja  ili kuchangia maendeleo na huduma kwa watoto wenye albinism na waishio mazingira magumu.
Wewe ni mdau muhimu sana na kama haujapata kadi ya mwaliko tafadhali piga simu namba 0767212428.
Huku tukitambua mchango wako tunatanguliza shukrani zetu za dhati tukiamini kuwa utapokea na kukubali ombi hili kwa lengo la kuboresha mazingira ya watoto hawa.

Nyote mnakaribishwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.