ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 7, 2015

MTANGAZAJI WA RADIO FREE AFRICA APETA KURA ZA MAONI UDIWANI CHADEMA, SASA KUSUBIRI KURA ZA UBUNGE.

Mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa William Bundala al-maarufu kwa jina la “kijukuu cha bibi” akiwa amebebwa juu na wakazi wa Ushetu.

SHINYANGA
MWANDISHI wa habari na mtangaaji wa Radio Free Africa William Bundala (KIJUKUU CHA BIBI K) ameshinda kura za maoni katika nafasi ya Udiwani katika kata ya Ulowa jimbo la Ushetu.

Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa uchaguzi huo Sangoma amesema kuwa Bundala ameshinda nafasi hiyo kwa kupata kura 46 dhidi ya Wagombea wenzake Charles Bahati aliyepata kura 14 na Marco Matheo ambaye hakupata kura yoyote katika kinyang’anyiro hicho.

Kuelekea uchaguzi mkuu Bundala alitangaza nia ya Kugombea Ubunge katika jimbo la Ushetu na udiwani katika kata ya Ulowa huku akisimamia kauli mbiu yake kuwa “Tunahitaji mawazo na nguvu mpya za vijana kuleta mabadiriko ya maendeleo”.
Kulia ni mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa William Bundala al-maarufu kwa jina la “kijukuu cha bibi” anapokuwa kazini kikazi zaidi.

Akiongea kwa njia ya simu akiwa jimboni Bundala amesema kuwa huu ni mwanzo na kuongeza kuwa kwa sasa anasubiri kura za maoni za ubunge ili kuchaguliwa kupeperusha bendera ya Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Sambamba na hayo Bundala amesema kuwa Tanzania ilipofikia kwa sasa inahitaji viongozi wazalendo wenye uchungu na rasilimali za wananchi na siyo kiongozi mwenye uchu wa madaraka anayetaka uongozi kwa rushwa.

Kwa upande wao wagombea waliokuwa katika kinyang’anyiro hicho cha udiwani wamesema kuwa wameridhika na matokeo na kwamba lengo la CHADEMA ni moja kuleta mabadiriko katika jimbo la Ushetu na kata ya ulowa kwa Ujumla.



Kwa sasa Bundala anasubiri kura za maoni za Ubunge zinazotarajiwa kufanyika wiki ijayo huku akiwa katika kinyang’anyiro hicho na watia nia wengine wawili ambao ni Mabula Nkwabi na John Kitibu ambaye alipata kura 45 katika kura za maoni za jimbo la Kahama Mjini katika uchaguzi ambao James Lembeli aliibuka mshindi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.