Mkuu wa Huduma za Rejareja wa benki hiyo, Francois Botha akiongea machache wakati wa ufunguzi rasmi tawi la benki ya First National la Mbezi Beach jana jijini Dar es salaam. |
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akitoa shukrani zake za pekee kwa benki ya First National kwa kuendelea kufungua matawi yake pembezoni mwa mji wa Dar es Salaam ambapo alisema ni jambo la faraja sana pale mteja anapofuatwa alipo na si kila siku kukimbilia kufungua benki katikati ya mji. |
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (wa pili toka kulia) akiwa na Balozi wa Heshima wa Djibouti Said Shamo ( kwanza kulia) pamoja na viongozi wa benki ya First National. Kulia ni Mkuu wa Huduma za Rejareja, Francois Botha na Mkuu wa Bidhaa na Huduma za Mitandao, Silvest Arumasi. |
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiongea machache na mmoja ya kiongozi wa Benki hiyo. |
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya First National na wageni waliohudhuria uzinduzi huo. |
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Huduma za Rejareja wa benki hiyo, Francois Botha. |
“Mara kwa mara tunafikiria mbinu mpya za kutuwezesha kutoa huduma inayowapa unafuu wateja wetu kwa kupeleka huduma hiyo karibu na makazi pamoja na biashara zao. Tawi hili litarahisisha huduma kwa wateja wetu wanaoishii Mbezi na maeneo ya jirani ambayo yana biashara nyingi zinazokua kwa kasi,” alisema Botha.
Mkuu wa kitengo cha bidhaa na huduma za kidigitali wa First National Bank, Silvest Arumasi, alisema kuwa kutokana na ukuaji wa kasi wa jiji la Dar es salaam benki hiyo imeona umuhimu wa kuhakikisha huduma za kisasa za kibenki zinawafikia watu wengi zaidi.
“Tunataka kuhakikisha tunatoa mchango muhimu katika kuendeleza sekta ya fedha nchini na tumepanga kuendelea kuanzisha huduma mpya zenye ubunifu na za kitaalamu hapa nchini,” alisema Arumasi.
Tawi hilo lililofunguliwa Mbezi Beach Shamo Towers litatoa huduma za kibenki mahususi kukidhi mahitaji ya watumiaji huduma pamoja na wafanyabiashara katika eneo hilo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.