MARA baada ya Cha cha mapinduzi CCM kuzinduliwa kampeni zake za uchaguzi kitaifa ndani ya jiji la Dar es salaam viwanja vya Jangwani, mbio za kampeni sasa zinaendelea kwenye mikoa mbalimbali hapa nchini ambapo mkoa wa Mwanza unategemea kufanya uzinduzi wake kesho (jumatano) ya tarehe 26 August 2015 na mgeni rasmi anatazamiwa kuwa Mjumbe wa NEC Livingstone Lusinde maarufu Kibajaji ambaye ni mbunge wa Mtera.
Kwa mujibu wa Katibu uenezi wa CCM Mkoa wa Mwanza Simon Mangelepa amesema kuwa uzinduzi huo utafanyika katika viwanja vya Mbugani wilayani Nyamagana kuanzia saa sita mchana hadi saa 12 jioni ambapo maandalizi yote yamekwisha kamilika.
Ameongeza kuwa Mhe. Lusinde ataambatana na mwenyeji wake katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza pamoja na viongozi wengine waandamizi wa chama hicho kuwatambulisha madiwani wateule 19 wa wilaya ya Nyamagana na 18 kwa wilaya ya Ilemela
Majimbo mengine yaliyoalikwa kwenye uzinduzi huo ni pamoja na Magu, Sengerema, Ukerewe, BOFYA PLAY KUSIKILIZA.
Vipi kuhusu taarifa zilizoenezwa kipindi cha ziara ya mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA (UKAWA) Edward Lowassa zikimtaja katibu huyo mwenezi mkoa wa Mwanza (Simon Mangelepa) pamoja na mwenyekiti wake Anthony Diallo, kuwa wangekihama chama hicho na kujiunga CHADEMA ikiwa ni pamoja na kutambulishwa kwenye mkutano uliopita wa kuomba wadhamini kanda ya ziwa zinaukweli kiasi gani. Bwana Mangelepa alijibu ...(BOFYA PLAY KUSIKILIZA) (SAUTI KUWAJIAHIVI PUNDE.....
Busungu Aingia Rasmi Kinyang’anyiro cha Urais 2025
-
*Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya
Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa
kuwa Mgo...
ONE NATION, ONE DREAM: OCTOBER TUNATIKI !!
-
Saturday, 09th August 2025
Christopher Makwaia
Tel: +255 789 242 396
In Dodoma, with skies so bright,
President Samia Suluhu Hassan steps forth, re...
Nondo Oscar Awasha MOTO wa Ubunifu kwa Vijana"
-
*Mfugaji na mfanyabiashara wa mbwa, Nondo akionyesha moja ya mbwa anaowauza*
Na Woinde Shizza, Arusha
Mfugaji na mfanyabiashara wa mbwa, Nondo Oscar, ...
Ndege 10 kubwa zaidi za kijeshi duniani 2025
-
Ndege kubwa ya kijeshi ni muhimu kwa kusafirisha askari, vifaa, magari ya
kivita, na misaada ya kibinadamu. Uwezo wa kubeba mizigo, urefu wa ndege,
na ukub...
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.