Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akijiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia mfumo mpya wa kielektoniki(Biometric Voters Register( BVR) katika kijiji cha Msoga,kata ya Msoga wilayani Bagamoyo leo.Kulia akiangalia kwa makini ni mwandikishaji msaidizi Bi.Happyness Thomas Misana na katikati ni Afisa TEHAMA kutoka ofisi Tume ya Taifa Uchaguzi Bi.Mariam Rajabu.Kushoto aliyesimama akishuhudia ni Mbunge wa Chalinze Ridhwani Kikwete.
Afisa TEHAMA kutoka ofisi ya Tume ya Uchaguzi Taifa ya Uchaguzi Bwana Sanif Khalfan akichukua lama za vidole vya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais alipokwenda kujiandikisha kijijini kwake Msoga wilaya ya Bagamoyo leo .
Bwana SANIF Khalfan ambaye ni Afisa TEHAMA kutoka ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi akimpiga picha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais alipokwenda kujiandikisha kupiga kura kwa kutkumia teknolojia mpya ya BVR kijijini Kwake Msoga leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitambulisho chake wakati wa zoezi la kujiandikisha kijijni kwake Msoga leo.
Mwenyekiti wa tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kitambulisho chake cha kupiga kura baada ya Rais Kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya BVR huko kijijini Msoga wilayani Bagamoyo leo.
Rais Kikwete akimshukuru Mwenyekiti wa tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva baada ya kukabidhiwa kitambulisho chake cha kupiga kura baada ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya BVR huko kijijini Msoga wilayani Bagamoyo leo. Picha na Freddy Maro.
Rais akuonyesha kitambulisho chake alichopewa mara baada ya kujiandikisha katika daftari daftari la kudumu la
wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya BVR huko kijijini Msoga wilayani
Bagamoyo leo.
---
JUMLA ya watu milioni 11,248,194 wameandikishwa kwenye daftari la
kudumu la wapiga kura zoezi ambalo linaendelea kwa sasa hapa nchini
likiwa limeingia mkoani Pwani.
Hayo yalisemwa leo
kwenye Kijiji cha Msoga kata ya Msoga wilayani Bagamoyo na mwenyekiti wa
Tume ya Uchaguzi ya Taifa Damian Lubuva alipokuwa anampa taarifa Rais
Dk Jakaya Kikwete mara baada ya kujiandikisha.
Bw.
Lubuva alisema kuwa malengo ni kuandikisha watu milioni 21 hadi 23 kote
nchini mara zoezi hilo litakapokamilika kati ya Julai mwishoni au Agosti
mwanzoni kama hakutatokea matatizo.
“Hadi sasa ni
mikoa 11 inaendelea na zoezi ambayo ni Mwanza Shinyanga, Geita, Simiyu,
Mara, Manyara, Arusha, Kilimanjaro Morogoro na jana ulianza mkoa wa
Pwani,” alisema Lubuva.
Aidha alisema kuwa changamoto
zilizojitokeza ni za kawaida hasa kutokana na mfumo huu kuwa ni mpya
kwani kila jambo jipya lina changamoto zake.
“Mfumo
huu ni mpya hivyo lazima kuwe na changamoto za hapa na pale lakini zoezi
linakwenda vizuri na tunaamini kuwa tutafanikiwa kama tulivyopanga,”
alisema Lubuva.
Mkoa wa Pwani una jumla ya vituo 1,752
na mashine za BVR 932 ambapo kata ya Msoga kuna jumla ya vituo 17 zoezi
hilo kwa mkoa wa Pwani lilianza jana na litamalizika Julai 20.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.