Airtel Fursa yazinduliwa na warsha mkoani Mwanza Jijini Mwanza Tarehe 7 July Meya Stanslaus Mabula amezindua warsha maalum kwa vijana ya 'Airtel Fursa' kutoka Airtel Tanzania wenye lengo la kuwawezesha Vijana.
Akiongea katika ufunguzi wa warsha hiyo na uzinduzi wake alisema, mpango huu wa Airtel Fursa ni mzuri na umekuja kwa wakati sahihi na kuwawezesha vijana kwa kuwapa vifaa ili kuboresha biashara zao "Wote tunajua tatizo kubwa linalowasumbua vijana kwa sasa.
Wengine wanaelimu nzuri lakini bado hawajapata ajira hivyo Airtel Fursa imekuja kusaidia. Najua si rahisi kufikia vijana wote kwa wakato mmoja lakini warsha tunayoanza leo ni mwanzo mzuri hivyo nawasihi vijana wengi iwezekanavyo kuomba kujiunga na mpango wa 'Airtel Fursa' na kama wakichaguliwa wawe miongoni mwa walionufaika na mpango huu na kuupa sifa mkoa wetu kwa kuleta mabadiliko", alisema Amewasihi vijana wa jiji hilo kuitumia nafasi hiyo kwa kuonyesha ubunifu na kuhakikisha wanakua kwenye hali ya kupongeza Airtel kwa
nafasi waliopata.
"Tunajisikia heshima kwa kuteuliwa kuwa mkoa wa pili baada ya Dar Es Salaam ambapo ulifanyika mwezi uliopita na kunufaika na mradi huu wa Airtel Fursa na hiyo inaonyesha jinsi Airtel inavyojitolea kwa ajili ya kuhudumia jamii. Tunawashukuru kwa kuiunga mkono serikali kwa kutengeneza ajira na kupunguza umasikini", alisema Meya Mabula
Alisema Mwanza kunavipaji vingi hivyo vijana wanaweza kutumia nafasi hiyo kuboresha maisha yao na kukuza uchumi wa Mwanza. "Huu sio wakati wa kusubiri wakati kunanafasi nyingi, vijana wetu wanatakiwa kujihusisha na shughulu mbalimbali zitakazowafanya wanufaike na mpango huu wa Airtel Fursa" alisema
Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema, "Airtel Fursa ni moja ya huduma za jamii kutoka Airtel na kuwataka vijana kujiunga na mradi huo".
Alisisitizia vijana kuwa sio tu wanaojiunga ndio watakaonufaika na Airtel Fursa bali pia mpango huo utatoa mafunzo kwa vijana zaidi ya 1500 kila mwaka nchi nzima kupitia warsha kama hii iliyofanyika Mwanza katika Ukumbi wa Jiji (City Hall) kwa lengo la kuwawezesha vijana kujijenga na kujitegemea kwa kupatiwa mafunzo kwenye usimamizi wa fedha, upatikanaji wa mikopo, kufungua akaunti ya benki na mambo muhimu katika kuendesha biashara.
Airtel Tanzania imedhamiria kufanya kazi na Serikali ili kuhakikisha vijana wanaangaliwa na wanaamini mpango huu utaleta mabadiliko makubwa na yakushangaza kwa vijana wa Mwanza na maeneo mengine yatakayofikiwa na mpango huu wa Airtel Fursa.
Mmoja wa vijana washiriki wa 'Airtel Fursa' Emmanuel Benjamin akifunguka. |
Darasa la 'Airtel Fursa' |
Wadau toka Airtel Tanzania |
Mmoja wa vijana washiriki wa 'Airtel Fursa' Elina Elikana akichangia. |
Mambo ya kuzingatia. |
Kwa umakini. |
Vijana ya'Airtel Fursa' Mwanza. |
Meya Stanslaus Mabula akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Airtel mara baada ya kuzindua warsha maalum kwa vijana ya'Airtel Fursa' kutoka Airtel Tanzania. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.