Baadhi ya waajiriwa wapya wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wakiwa katika mafunzo ya awali (Induction course) yanayofanyika katika Hoteli ya Kingsway Mkoani Morogoro. |
Baadhi ya waajiriwa wapya wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wakiwa katika mafunzo ya awali (Induction course) yanayofanyika katika Hoteli ya Kingsway Mkoani Morogoro. |
Baadhi ya waajiriwa wapya wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wakiwa katika mafunzo ya awali (Induction course) yanayofanyika katika Hoteli ya Kingsway Mkoani Morogoro. |
Baadhi ya waajiriwa wapya wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wakimsikiliza kwa umakini Kaimu Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Jasper Mero (hayupo pichani). |
Kaimu Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Jasper Mero (Kushoto) akisisitiza jambo wakati akijibu maswali mbalimbali ya waajiriwa wapya wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi. |
Na
Saidi Mkabakuli
WATUMISHI
wa umma nchini wameaswa kuwa waadilifu na kuzingatia ubora wa kazi wakati
wanatoa huduma kwa wananchi.
Wito
huo umetolewa na Kaimu Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bw.
Jasper Mero wakati akifungua mafunzo ya awali ya wiki moja kwa waajiriwa wapya
130 wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi
yanayofanyika katika Hoteli ya Kingsway mkoani Morogoro.
Bw.
Mero amesema kuwa udilifu na ubora kwa watumishi wa umma ni kinga dhidi ya
matumizi mabaya ya ofisi za umma na ni moja kati ya njia zinazowawezesha
watumishi wa umma kuwa wachapakazi hodari.
“Ofisi
ya Taifa ya Ukaguzi inaamini katika “Ubora”kwa kila inachokifanya ukianzia
ubora wa taarifa za ukaguzi zinazotolewa, huduma bora kwa wadau wake, ubora wa
watumumishi kwa maana ya taaluma, maadili, weledi,” alisema Bw. Mero.
Ameongeza
kuwa Falsafa hii ya ubora ndiyo iliyoifanya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kupata
umaarufu mkubwa kikanda na Kimataifa.
“Kiwango
cha juu cha Ubora wa kazi zetu na utendaji wa kazi unaozingatia weledi vitaweza
tu kufikiwa kwa kuajiri watumishi wenye sifa stahiki, maadili, na bidii ya
kuchapa kazi na wanaoweza kwenda sambamba na kasi kubwa ya mageuzi katika Ofisi
ya Taifa ya Ukaguzi,” aliongeza Bw. Mero.
Akizungumza
wakati wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Ofisi hiyo,
Bw. Gerald Mwanilwa alisema kuwa mafunzo elekezi ni matakwa ya Kanuni za Kudumu
za Utumishi wa Umma za mwaka 2003, hususani Kanuni Na.103 (1-6) pamoja na
Kanuni za kudumu za Utumishi Serikalini za 2009 Kifungu G.3 (a na b).
“Mafunzo
haya ni kwa mujibu wa matakwa ya kisheria na yanalenga kutoa uelewa mahususi
kwa waajiriwa wapya kulingana na kada zao,’ alisema.
Kwa mujibu wa Bw.
Mwanilwa, kupitia mafunzo hayo, washiriki wataweza kuelewa namna ya kutekeleza
majukumu yao kama Watumishi wa Umma pamoja na kupata fursa ya kujifunza
Miongozo na Nyaraka mbalimbali watakazozitumia kama watumishi wa umma na wafanyakazi
wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali.
Pia, kupitia mafunzo hayo
watapata fursa ya kujifunza na kuelewa utamaduni wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi
unaosisitiza kufanya kazi kwa uweledi, uadilifu na kwa kuzingatia ubora na
viwango vya kitaifa na kimataifa ambapo ofisi yetu ni Mwanachama (Intosai
Afrosai na Afrosai-E).
“Mafunzo
haya ni ya wiki moja yatatoa fursa kwenu kujua maana ya kuwa mtumishi na kazi
za mkaguzi na miiko au maadili yake. Pia mtaelezwa kwa kifupi na kupewa
utangulizi kuhusu Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, sheria mbali mbali, Kanuni na
taratibu ili kuwawezesha kuelewa na kufanyakazi kama watumishi wa umma,”
aliongeza Bw. Mwanilwa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.