ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, July 26, 2015

UKAWA WAKIMPA LOWASSA TIKETI WATAISHINDA CCM?

Kuna Msemo wa MayanÅ› wa Kale sana Usemao, Kama Tiger akipewa mbawa za kuruka na Tai Akikataa atakuwa mpumbavu. Kosa la CCM kuchakachua bunge la katiba liliwafanya Upinzani Tanzania Kufanya Jambo la Kihistoria, kuunganisha Nguvu Pamoja. 

Na sasa wana Fursa nyingine ya Dhahabu, Kukatwa kwa Lowassa CCM, Kama wakimpa Lowassa Tiketi, Ukawa watakuwa wamejizolea wapigakura maradufu. 

Ni wazi zaidi ya Mamilioni wa CCM waliomtaka Lowassa wataleta Kura zao Ukawa.

WASEMAVYO MAKOMENTA.


+Thobias Marandu Presentataion yajko hii inakuonyesha kama mtu mbabaishaji na ushauri wako huu ni wa hisia zako binafsi ambazo hazilengi kuwanufaisha watanzania kwa sababu  unasahau  mambo manne: (1) La kwanza ni kuwa huko CCM Malecela naye alienguliwa kwa njia hiyo hiyo mwaka 2005 ambayo ilimleta Kikwete. Lowasa alikuwa ni sehemu ya Team Kikwete na wala hakulalamika. (2) La pili ni kuwa Ukawa inapata sifa sana leo kwa sababu  moja ya kupambana na ufisadi wakati Lowasa mwenywe akiwa ni mmoja wa mafisadi hao waliotajwa na CHADEMA pale Mwembeyanga. (3) Lowasa is power hungry. Kama Lowasa ana nia njema na nchi hii, siyo lazima yeye ndiye awe mgombea wa urais, anaweza kumsapoti mgombea anayemwanini kama Nyerere alivyofanya mwaka 1995. Ila yeye kutaka ndiye awe Rais ni tamaa ambayo sikubaliani nayo. Lowasa ni used and exhausted material ambaye hawezi kumudu majukumu makubwa ya urais kwa miaka mitano ijayo. (4) Maovu yote unayosema kuhusu CCM yamefanyika wakati Lowasa akiwa ndani ya CCM tena akiwa very influential lakini akikaa kimya; je hakuyanona wakati huo hadi pale alipoenguliwa kwenye kinyang'anyiro cha uraisi?? Ni afadhali sana kubaki na CCM bila Lowassa kuliko kuwa na UKAWA yenye Lowassa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.