Askofu wa kanisa Katoliki jimbo la Kahama Ludovick Minde amewataka wazazi na walezi kuwalea watoto wao katika misingi ya dini sanjari na kuwapeleka shule za kichungaji ili waweze kuwa watawa na mapadri ili kanisa liweze kuendelea kuwa na viongozi waadilifu.
Kauli hiyo imetolewa jana na Askofu huyo hafla ya upadrisho kwa waliokuwa mashemasi wawili ambao ni Padri Justine Bahati kutoka Parokia ya Mbogwe na Padri Endrew Lupondya kutoka Parokia ya Nyasubi mjini Kahama.
Amesema kuwa watoto wengi wamekuwa na ndoto za kuwa watumishi wa mungu lakini zao zimekuwa zikiyeyuka kutokana na malezi duni ya wazazi ambao hawawalei katika misingi hiyo ya kumtumikia mungu na hivyo kanisa kuendelea kukosa mapadri.
Aidha amewataka mapadri ambao wamepadirishwa kuhakikisha wanafanya kazi ya kanisa ili kuliendeleza taifa la Mungu na kuwataka wawatendee mema watu na wasichoke kulihubiri neno la Mungu popote pale duniani.
Wakitoa shukrani zao kwa Askofu Minde mapadri hao wateule wamesema kuwa haikuwa kazi rahisi kufikia daraja la Upadri na kusema kuwa Mungu mwenyewe ndiye amesaidia kufikia hatua hiyo na kuahidi kuitendea haki hatua hiyo waliyofikia.
Wameongeza kuwa wanawashukuru wazazi wao wa kimwili na wazazi wa kiroho kuendelea kuwatia moyo katika safari yao ya utume na kwamba ndio mwanzo wanajiandaa kumtumikia Mungu kwa kuchunga kondoo wake.
Hata hivyo wamesema kuwa kazi ya utume inahitaji maombi ya kila mwumini na ili waweze kuitimiza wanahitaji msaada wa waumini na viongozi wao ambao walitangulia waweze kuifanya na kuitimiza.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.