ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, July 22, 2015

KUELEKEA UCHAGUZI 2015 GHAFLA CHADEMA YASISIMUA MWANZA.

Jiji la Mwanza hii leo limesimama kwa dakika kadhaa kupisha shamrashamra za maandamano zilizoambatana na Mkutano wa CHADEMA uliofanyika jijini hapa ukiwa na lengo la kutambulisha baadhi ya wabunge walio hama CCM na kukimbilia chama hicho (Lembeli na Ester Bulaya) sanjari na watu wakitegemea kusikia jina la mgombea kiti cha urais ambaye awali alitajwa kuwa angetambulishwa kupitia mkutano huo.

Mamia ya wanachama na wafuasi wa chama hicho wamehudhuria mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa Magomeni kirumba jijini Mwanza kisha baadaye kwa maandamano wakawasindikiza viongozi wao hadi hoteli walizofikia.

Umati unaoonekana hapo juu 'kideoni' ni kutoka hoteli ya Gold Crest ukiwasindikiza viongozi walio fikia hotelini hapo.
Katibu mkuu wa CHADEMA W. Slaa akihutubia makumi kwa mamia ya wananchi na wanachama waliojitokeza leo kwenye viwanja vya Magomeni \kurumba jijini Mwanza.
Ze nyomi kwa area.
Katibu mkuu wa CHADEMA W. Slaa akihutubia makumi kwa mamia ya wananchi na wanachama waliojitokeza leo kwenye viwanja vya Magomeni \kurumba jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa Chama cha maendeleo na Demokrasia nchini (CHADEMA) Mbowe akihutubia makumi kwa mamia ya wananchi na wanachama waliojitokeza leo kwenye viwanja vya Magomeni kurumba jijini Mwanza.
Salum Mwalimu.
Mkutano huo pia uliwatambulisha wabunge walio hama CCM na kukimbilia chama hicho Ester Bulaya na Mbunge wa Kahama Mhe. Lembeli ambao walirudisha kadi zao na kukabidhiwa kadi mpya za CHADEMA.
Ester Bulaya na Lembeli wakikabidhiwa kadi zao.
Haya wamezaliwa upya ndani ya CHADEMA ni Ester Bulaya na Lembeli.
Hata hivyo bado ni kitendawili kuhusu mgombea wa urais kwa kiketi ya UKAWA kupitia muungano wa vyama vya upinzania ambavo ni Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF na NLD angetangazwa, lakini hakuna aliyetangazwa. 

Hadi sasa tarehe za kumtangaza mgombea huyo zimerushwa zaidi ya mara mbili huku mvutano ikiendelea ndani ya vyama hivyo. Gumzo lililopo je ni chama gani kitamtoa rais na mgombea mwenza?, Je mgawanyo wa ruzuku mwisho wa siku utakuwa?

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.