MWANAMUZIKI nyota wa muziki wa dansi, Ramadhani Masanja 'Banza Stone', amefariki
dunia.
Banza amefariki dunia alipokuwa amelazwa katika Hospitali ya
Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Mwanamuziki huyo nyota wa zamani wa Twanga Pepeta na Tot alikuwa
amelazwa hospitalini muda mrefu.
Mmiliki wa Twanga Pepeta, Asha Baraka amethibitisha kifo cha Banza
Stone.
“Kweli amefariki leo saa saba, baada ya kutoka tu msikitini ndiyo
tumepata taarifa hizo za msiba,” alisema Asha Baraka.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.