HOTUBA YA KAIMU KATIBU TAWALA MKOA WA
MWANZA WAKATI WA KUFUNGUA MASHINDANO YA NGAZI YA MKOA YA MICHEZO YA SHULE ZA
SEKONDARI TANZANIA (UMISSETA) NSUMBA SEKONDARI TAREHE 23 MEI, 2015
Awali ya yote napenda
kuchukua fursa hii kukushukuru Katibu Tawala Msaidizi ambaye ni Afisaelimu wa
Mkoa na Viongozi wenzako katika seksheni ya Elimu kwa kunialika kufungua Mashindano
haya ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA).
Nimeupokea mwaliko huu kwa
furaha kwa vile umenipa fursa ya pekee kuwaona na kuzungumza na hadhara hii ya
wanafunzi, Wanamichezo na Walimu wao.
Aidha, nitumie fursa hii kuupongeza uongozi wa Nsumba na Jumuia yote kwa
maandalizi mazuri ya Mazingira kwa ajili ya mashindano haya. Ahsanteni sana.
Ndugu
Viongozi na Wanamichezo:
Leo tukumbushane umuhimu wa
Michezo kwa Taifa na kwa mwanamichezo, mashindano haya ni nyenzo mojawapo ya
kujenga Umoja wa Kitaifa na hivyo kufanya maelewano na mshikamano kwa Watanzania. Michezo ni Burudani lakini kwa sasa
kutokanana mabadiliko ya Mazingira ya Kisiasa, Kiuchumi na Kijamii, Michezo ni
Kipaumbele katika kutoa pia Ajira kwa vijana wetu, kukuza Biashara na kujenga jamii bora yenye maelewano. Kwa mfano, Nchi za wenzetu za Ulaya na
Marekani, lakini nchi zingine za Afrika za Mataifa kama Nigeria, Togo, Ivory
Coast, Cameroon zinatumia kikamilifu nafasi hii ya Michezo kujitangaza kiuchumi na kijamii.
Natambua kwamba ninyi ni
Wanafunzi ambao mnahitaji kukuza Taaluma na vipaji vyenu. Moja ya nafasi hizo
ni Michezo ili michezo iendelee kukua nchini, ni lazima ukuzaji wa vipaji vya
michezo uanzie shuleni, ndiyo maana michezo ni sehemu ya Mtaala wa masomoyenu,
kama ambavyo tunawataka mfanye bidii katika masomoyenu, fanye bidii pia na
kukuza vipaji vyenu katika michezo kwa kushiriki kikamilifu kuonesha ubunifu.
Wanamichezo bora, ni Watu
wasikivu, wenye nidhamu na watiifu.
Ninyi vijana ambao ndio viongozi wa kesho wa Taifa letu mnahitaji sana
kujijengea nidhamu na maadili yahali ya juu ili muweze kuendana na hali ya maisha
ya ushindani yatakayokuwa yanawakabili.
Nidhamu, inamuwezesha Mtu kufanya kazi zake kwa mpangilio mzuri
unaofuata taratibu zote za kazi kwa wakati.
Hii ndiyo njia ya uhakikika ya kufikia malengo yoyote yale na kupata
mafanikio.
Aidha, kwa njia ya Michezo,
nidhamu shuleni itaongezeka na matarajio yetu ni kuwa nidhamu hiyo itajitafsiri
pia katika matokeo mazuri kwenye
Taaluma. Matarajio ni kuwa, wanafunzi
watakuwa na mahusiano mazuri zaidi kati yao na walimu wao na wale wote
wanaopata Burudani ya Michezo. Ama tunatarajia
kuwa wataendelea kuwa watu wenye Nidhamu katika Utu Uzima wao, ili hatimaye
tuwe na Taifa la Watu wenye nidhamu ya kutolewa mfano.
Ndugu
Wanamichezo,
Nitumie fursa hiipia
kuwakumbusha kwamba mnapofurahia kushiriki katika Michezo hii, ni lazima mkumbuke
kuwa furaha yenu itandelea kudumu kama mtatambuakuwa kuna mpinzani
mkubwa kati yetu aitwaye Virusi vya UKIMWI na UKIMWI. Kila mmoja wenu anaelewa vya kutosha juu ya
Adui huyu. Ni wajibu wangu kama Kiongozi
na Mlezi wenu kuwakumbusha juu yahatari inayowakabili msipokuchua tahadhari ya
kutosha. Kumbukeni UKIMWI bado unaenea
kwa kasi kubwa sana hasa miongoni mwa Vijana wa Rika lenu kuliko rika lolote
jingine. Niwakumbushe kwamba upingine
kwa nguvu zote Ugonjwa huu.
Msikubali kukatishwa masomo na msikubali kutenganishwa mapema na familia
zenu. Kwenu ninyi, njia bora pekee ni
kusubiri hadi wakati muafaka wa ndoa.
Wekeni bidii katika masomo, kwani muda ukifika yote yatajipanga vizuri.
Ndugu
Wanamichezo,
Nimeelezwa kuwa baada ya
Michezo hii yapo Mashindano ya Kanda ya Ziwa ambapo Mikoa ya Mwanza, Mara na
Simiyu hukutana ili kuimarisha mahusiano ya Vijana wa Shule za Sekondari na
kuunda timu moja ya Kanda. Ni muhimu
timu zetu zijipange kushiriki vizurina kutuletea ushindi wa kishindo. Aidha timu hizo ziandaliwe vizuri ili zikashiriki
kama washidani na si wasindikizaji. Kushiriki kwenu kunatujengea heshima katika kujenga upeo wa akili za vijana wetu na
kujenga mahusiano mazuri ya kikanda.
Natoa rai kwa Mashirika, Vyama vya Michezo na watu wengine kushiriki kwa
kuchangia kufanikisha ushindi wa timu zetu za Mkoa.
Ndugu
Wana Michezo,
Nimalizie hotuba yangu kwa
kuwatakia kila la kheri kwa kipindi chote cha mashindano, aidha msisite
kuwasilianana ofisi yangu pale mtakapoonakuna ulazima wa kufanya hivyo kwa ushauri na maelekezo kwa ajili ya kuboresha
michezo hii.
Michezo hoyeeeeee!!!!
Asanteni
kwa kunisikiliza
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.