NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
MASHINDANO ya Koka Cup ngazi ya kata bado yanaendelea kutimua vumbi katika maeneo mbali mbali ambapo katika siku ya jana katika kata ya kongowe mchezo wa fainali umepigwa kwa kuzikutanisha timu ya Kongowe Fc ambao walemenyana na timu ya Mwambisi.
Katika mchezo huo wa fainali uliofanyika kwenye uwanja wa ungindoni Kibaha,timu ya Kongowe Fc ndio walioweza kutoka kifua mbele na kutawazwa na ubingwa baada ya kufunga wapinzani wao timu ya Mwambisi kwa mabao 2-1.
Mchezo huo wa aina yake uliweza kuvuta hisia za mashabiki walihudhuria katika mtanange huo kutokana na timu zote mbili kuwa na wachezaji mchanganyiko ambao baadhi yao wameshawahi kushiriki katika michuano mbali mbali hivyo mchezo huo kuwa wa upinzani wa hali ya juu katika kipindi chote.
Timu ya kongowe Fc ndio waliokuwa wa kwanza kuifumania nyavu za wapinzani wao kupitia kwa mshambuliaji wao mkongwe Emmanuel Bruno baada ya kuachia shuti kali lililoama kimiani baada ya kumshinda mlinda mlango wa Mwambisi Tabu Selemani na mpira huo kuzama langoni.
Hata hivyo wachezaji wa kikosi cha atimu ya Mwambisi hawakuweza kukata tama kutokana na kuingia kwa bao hilo na wao walijipanga na kuongeza mashambulizi ya gafla katika lango la wapinzani wao na kufanikiwa kuandika bao la kusawazisha katika dakika ya 12 lililopachikwa na Ansi Ansi.
Kadiri ya muda ulivyokuwa unazidi kwenda mchezo huo ulizidi kushika kasi kwa wachezaji wote wa timu mbili kufanya mashambulizi ya zamu kwa zamu lakini hadi kipenga cha kipindi cha kwanza kinapulizwa timu zote zilikwenda mapumziko zikiwa zimetoshana nguvu sawa ya kufungana bao 1-1.
Katika kipindi cha pili wachezaji wa Kongowe Fc walionekaana kuingia na mipango mipya ya kutaka kupata bao ambao juhudi zao ziliweza kuleta mafanikio baada ya kuandika bao la pili katika dakika ya 82 kwa njia ya mkwaju wa penati lililofungwa kiufundi na mchezaji Jese Joseph kwa guu lake la kushoto na kufanya hadi dakika 90 zinamalizika kongowe fc kutoka kidedea kwa mabao 2-1 dhidi ya wapinzani wao.
Pia katika mchezo huo ambao ulionekan akuhudhuriwa pia na wakinamama na wakinadada wengi kupita wakinababa uliweza kuzua gumzo katika kipindi cha kwana katika dakika za 28 mpaka mapumziko kutokana na kuibuka kwa mvua ya gafla uwanjani hapo hali ambayo iliweza kuwaacha midomo wazi mashabiki kwano maeneo mengine kulikuwa ni kukavu hakuna mvua isipokuwa maeneo ya uwanjani tu.
Kwa ushindi huo timu ya Kongowe fc ambao walikuwa mabingwa mabingwa wa michuano hiyo ya koka cup ngazi ya Kata ya Kongowe iliyokuwa ikichezeshwa kwa mfumo wa ligi walizawadiwa shilingi laki tatu na ngao, mshindi wa pili ungindoni fc shilingi laki mbili na ngao,na mshindi wa tatu timu ya Mbambisi ilizawadiwa shilingi laki moja na ngao.
Mwandaaji wa michuano hiyo ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestery Koka alisema kwamba nia yake kubwa baada ya kumalizika kwa ngazi ya kata michuano hiyo itaendelea katika ngazi ya Wilaya ambapo kila kata itatoa washindi wawili watakaokutana katika hatua ngazi ya Jimbo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.