NA. ALBERT G. SENGO MWANZA
MKUTANO Mkuu wa Klabu ya Toto Africans ya jijini Mwanza umefanyika leo Jumapili na kupitisha maazimio ya kuiondoa madarakani Kamati tendaji na Sekretarieti yake ikiwa ni pamoja na kumsimamisha Makamu Mwenyekiti wake na kuteua Sekretarieti mpya.
Kamati hiyo ya utendaji pamoja na Sekretarieti yake walishindwa kuwasilisha ripoti ya mapato na matumizi ya Klabu ya Toto Africans kwa kipindi cha mwaka mmoja 2014-2015 na yale yote yaliyojiri katika mchakato wa kuelekea Ligi kuu soka Tanzania Bara ambapo humo inasemekana kuwa kulikuwa na ufujaji mwingi wa fedha na matumizi binafsi zaidi ya matumizi ya kawaida ya klabu kutoka fedha za wawezeshaji sanjari na vyanzo vya uwekezaji vya klabu.
Mapema leo Uongozi, Kamati na Sekretarieti iliyosimamishwa ilishindwa kuhudhuria mkutano huo bila kutoa sababu na hata maandalizi ya mkutano kama yalivyo agizwa hayakufanywa ambapo awali mkutano ulikuwa umepangwa kufanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya jiji badala yake wanachama wakaamua mkutano huo ukafanyike kwenye eneo la wazi uwanja wa Nyamagana Mwanza.
Isaac Wakuganda ni Msemaji mpya wa klabu hiyo anafunguka yale yaliyojiri... (BOFYA PLAY KUSIKILIZA KILICHOJIRI)
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.