JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA
KUHUSU
KAMPENI YA UGAWAJI WA DAWA ZA KUKINGA NA KUTIBU MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI
KIPAUMBELE KATIKA MKOA WA MWANZA
Ndugu Wananchi,
Magonjwa
yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, hususan Kichocho na Minyoo ya tumbo yameathiri
sehemu kubwa ya jamii katika mkoa wetu wa Mwanza. Magonjwa haya huleta
mahangaiko makubwa kwa wananchi hasa kwa
watoto ikiwemo upungufu wa damu, kuzorotesha ukuaji, kupunguza mahudhurio ya
watoto shuleni na pia kutofanya vizuri katika masomo yao. Ugonjwa wa Kichocho
husababisha Saratani ya Kibofu cha mkojo ambayo haina tiba hadi sasa. Minyoo ya
tumbo inaweza kusababisha Utumbo kuziba na mtu kulazimika kukatwa utumbo, Minyoo
ikiingia kwenye ubongo huleta dalili kama za kifafa vilevile minyoo huathiri Ini
na endapo muathirika hatawahi
kupata matibabu, dalili zote hizi
husababisha Mauti. Magonjwa haya ni moja kati ya vyanzo vikuu vya umasikini
katika familia, jamii, na taifa kwa ujumla. Aidha, takwimu zinaonesha kuwa
wagonjwa walioathirika kwa saratani ya kibofu cha mkojo na hasa wakazi wa kanda
ya ziwa kwa asilimia kubwa chanzo chake ni maambukizi ya kichocho.
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliridhia tamko la Shirika la Afya Duniani
linalokusudia kudhibiti au kutokomeza magonjwa haya ifikapo mwaka 2020, na ili
kutekeleza azma hiyo. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imetengeneza mpango
kazi wa miaka mitano wa Utekelezaji wa shughuli mbalimbali za udhibiti wa
magonjwa haya.
Ndugu Wananchi,
Tafiti
zilizofanyika mwaka 2005 zimeonyesha uwepo wa maambukizi ya ugonjwa wa Kichocho mkoani Mwanza yapo juu kuliko maeneo
mengine nchini. Utafiti huo ulionyesha maambukizi ya Kichocho yapo kati ya
asilimia 12.7 hadi 87.6 nchini. Utafiti huo unaonesha kwamba ugonjwa wa
kichocho umeenea zaidi maeneo ya kando kando ya ziwa Viktoria na kiwango cha
maambukizo ni zaidi ya 80% na kwa minyoo ya tumbo ni hadi 100%. Na katika jamii za watoto wenye umri wa
kwenda shule, tafiti kwa njia ya parasitologia, maambukizi ya ugonjwa huu ni
zaidi ya 50%. Kwa kiwango hicho cha maambuzi, kwa mujibu wa tafiti na maelekezo
ya kitaalam ya Shirika la Afya Duniani (WHO), jamii inapaswa ipewe dawa za
kukinga na kutibu.
Tangu
mwaka 2009 wizara ilizindua mpango wa udhibiti wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi
kipaumbele katika mikoa ya mitano kwa kuanzia, na hadi mwaka 2012 mpango huu
tayari ulikuwa umetekelezwa katika mikoa 14 na hadi mwishoni mwa mwaka jana
(2014) umekuwa ukitekelezwa katika mikoa
17 ikiwemo Mwanza iliyoingia katika mpango mwaka 2013. Hadi sasa, mpango huo unaratibu
shughuli zake katika mikoa 21 ikiwemo Kilimanjaro, Arusha, Simiyu na Geita
iliyoingizwa katika mpango mwaka huu wa 2015. Lengo la mpango kwa sasa ni kuifikia
mikoa ya Shinyanga, Mara na Kagera mapema iwezekanavyo ili kudhibiti magonjwa
haya ifikapo mwaka 2020.
Ndugu Wananchi,
Mkoa
unawajulisha wananchi na wakazi wote wa mkoa wa Mwanza kuwa tarehe 26 na 27 Mei 2015 tutaendesha kampeni ya ugawaji dawa za kukinga na kutibu magonjwa ya Kichocho
na Minyoo ya Tumbo. Walengwa wa kumeza dawa hizi ni watoto wote wenye umri wa kuanza shule ya msingi
walioandikishwa na wasioandikishwa.
Kampeni
hii itaendeshwa na watalaam wa huduma za afya wakishirikiana na Walimu katika shule
zote za msingi waliopatiwa mafunzo maalumu ya ugawaji wa dawa hizi. Kabla ya
unywaji wa Dawa hizi Mtoto anatakiwa ale chakula na katika muda usiozidi masaa 2 baada ya kula awe amepatiwa dawa
hizi; chakula hicho kitaandaliwa shuleni.
Hivyo
kila Mzazi katika mkoa wa Mwanza anaombwa amruhusu mtoto wake aende kumeza dawa hizi muhimu
ili ajikinge na kupata tiba ya magonjwa haya hatari kwani huduma hii ya dawa za kinga tiba inatolewa bila malipo
kwa kila mtoto.
Dawa
hizi zimethibitishwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuwa ni salama, na hazina
madhara yoyote kwa afya ya binadamu zinapomezwa kwa kufuata maelekezo yanayotolewa
na wahudumu wa afya na Walimu waliopatiwa mafunzo.
Dawa
zitakazohusika ni za Praziquantel za kudhibiti Kichocho na Albendazole za kudhibiti
Minyoo ya tumbo ambazo zitatolewa kwa
watoto wote wenye umri wa kwenda shule, walioandikishwa na ambao
hawakuandikishwa.
Ndugu Wananchi,
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.