“YENU BAA” YAIBUKA KIDEDEA SHINDANO LA FANYAKWELI KIWANJANI
Tarehe 23 Mei 2015 Dar es Salaam, Shindano la Tusker Fanyakweli Kiwanjani linaloendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti chini ya udhamini wa bia yake ya Tusker limempata mshindi wa pili wa Kampeni hiyo kiwanja cha “Yenu baa”. Baa hiyo maarufu inayopatikana maeneo ya Ubungo karibu na Wizara ya Maji imeibuka kidedea mara baada ya kupigiwa kura na wapenzi wengi wa bia ya Tusker kwa wiki iliyopita kupitia kipindi cha Ubaoni kinachorushwa na redio E-fm.
Baa hiyo ilipigiwa kura mara baada ya kuorodheshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti chini ya udhamini wa bia yake ya Tusker kwenye shindano hilo ambapo baa nyingine 9 zilichuana vikali kumpata mshindi wa wiki.
Mapema siku ya jumamosi, Kampuni ya bia ya Serengeti kwa udhamini wa bia yake ya Tusker ilifunga kambi maeneo ya Ubungo maji na kuporomosha burudani ya nguvu kwa wapenzi wa bia ya Tusker waliofika kuipongeza baa hiyo kwa ushindi walioupata.
Akiielezea baa hiyo kwa undani mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya tisheti na bia ya Tusker aliyojishindia wakati wa sherehe ya kuipongeza baa hiyo, mmoja wa wapenzi wa bia hiyo aliyefika kwenye eneo la tukio ambaye alifahamika kwa jina la Steven Mbele alisema...”Mimi nimeifahamu baa hii tangu mwaka 1993 kipindi hicho nilikua nasoma chuo kikuu cha Dar es salaam hapo mlimani na mara nyingi kila baada ya masomo mida ya jioni nilikua nakuja hapa na marafiki zangu kukata kiu, hivyo ubora wa huduma za baa hii ni tokea enzi za zile.” Bw. Mbele aliongeza kuwa amefurahishwa baada ya kusikia baa hiyo imeibuka na ushindi na kuipongeza Kampuni ya bia ya Serengeti kuanzisha shindano ambalo nia na madhumuni yake ni kuziinua baa za mitaa tunayoishi.
Washindi wengine waliojinyakulia zawadi mbalimbali kama;- mifuko, Tisheti na bia za bure ni pamoja na Alex Minja, Steven Thadei na Bi. Magret Mjema.
Akiongea na waandishi wa habari waliofika eneo hilo, Meneja Mauzo wa SBL kanda ya Ubungo Bw. Victor Mhindi alisema “Tunaipongeza “Yenu Baa” kwa kuwa mshindi wetu wa wiki nyinyi wenyewe ni mashahidi na mmejionea huduma za hapa jinsi wahudumu walivyo chap chap na wanavyofanya kazi kwa bidii”. Bw. Mhindi aliendelea kusema kuwa Kampuni ya bia ya Serengeti inajivunia kutoa sapoti kwa viwanja mbalimbali vya mitaa tunayoishi na kuwasihi wadau na wapenzi wa kinywaji cha Tusker kuendelea kuzipigia kura baa zinazoendelea kuorodheshwa kwenye shindano la Fanyakweli Kiwanjani ili kupata kilicho bora.
Naye Meneja wa baa hiyo Bw. Anselim Kimario ambaye hakusita kuimwagia sifa Bia ya Tusker alisema kuwa amefurahia zawadi ya fedha taslimu Tsh 100,000/= waliyopewa na mameneja wa Tusker baada ya kufanya kweli na kuongeza kuwa ushindi wao kama baa ya wiki umeongeza mauzo ya baa hiyo maradufu.
“Hiki ni kitu cha tofauti kwa kweli ninashukuru sana na niwapongeze sana mameneja wa Tusker kwa kutuandalia pomosheni hii ya Fanyakweli Kiwanjani kama mnavyoona baa yetu leo imechanganya kupita maelezo”.
Ili kuiwezesha baa ya mtaa unaoishi tembelea baa hiyo kisha burudika na kinywaji cha Tusker na piga picha nyingi uwezavyo na uipendekeze baa hiyo kwa kuweka picha hizo kwenye kurasa za jamii (Facebook na Twitter) za Tusker au kusikiliza kipindi cha Ubaoni kinachorushwa na redio E-fm kati ya saa tisa hadi moja usiku ndani ya siku za juma kwa maelezo zaidi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.